Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu-logo

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

United Nations

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Location:

New Rochelle, NY

Description:

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Twitter:

@HabarizaUN

Language:

Swahili

Contact:

9178215291


Episodes
Ask host to enable sharing for playback control

UNICEF Kenya - Elimu Jumuishi kupitia michezo: Watoto wenye ulemavu wa kuona wapate nafasi sawa

6/27/2025
Katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya viziwi wasioona, tunamulika hatua kubwa inayochukuliwa nchini Kenya katika kuhakikisha watoto wenye ulemavu wa kuona wanapata elimu bora na jumuishi. Mafunzo maalum yaliyofanyika jijini Nairobi yalileta pamoja wataalamu, walimu na mashirika ya maendeleo, kwa lengo la kuchochea elimu hiyo kwa njia ya michezo, kwa msaada wa Shirika la LEGO kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF Kenya. Sharon Jebichii na makala zaidi.

Duration:00:03:09

Ask host to enable sharing for playback control

Kilichotokea nchini Burundi 1972-1973 ni mauaji ya kimbari jumuiya ya kimataifa itambue hilo: Ndayicariye

6/27/2025
Serikali ya Burundi inataka mauaji yaliyofanyika nchini mwake kati ya mwaka 1972 hadi 1973 yatambulike kimattaifa kama ni mauaji ya kimbari dhidi ya Wahutu, je kwa nini wito huo umekuja sasa? Flora Nducha anatujuza zaidi

Duration:00:02:08

Ask host to enable sharing for playback control

27 JUNI 2025

6/27/2025
Hii leo jaridanitunaangazia msaada wa kibinadamu Gaza, na mauaji yaliyofanyika nchini Rwanda kati ya mwaka 1972 hadi 1973. Makala tunamulika inayochukuliwa nchini Kenya za kutekeleza haki za watu wenye ulemavu wa kutoona, na mashinani tunakwenda DRC, kulikoni?Hatimaye shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni, WHO limeweza kufikisha huko Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli, shehena ya kwanza ya vifaa vya matibabu ikiwa ni mara ya kwanza tangu tarehe pili mwezi Machi mwaka huu.Serikali ya Burundi inataka mauaji yaliyofanyika nchini mwake kati ya mwaka 1972 hadi 1973 yatambulike kimattaifa kama ni mauaji ya kimbari dhidi ya Wahutu, je kwa nini wito huo umekuja sasa.Katika makala leo ikiwa ni Siku ya Kimataifa ya viziwi wasioona, tunamulika hatua kubwa inayochukuliwa nchini Kenya katika kuhakikisha watoto wenye ulemavu wa kuona wanapata elimu bora na jumuishi. Mafunzo maalum yaliyofanyika jijini Nairobi yalileta pamoja wataalamu, walimu na mashirika ya maendeleo, kwa lengo la kuchochea elimu hiyo kwa njia ya michezo, kwa msaada wa Shirika la LEGO kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF Kenya.Na mashinani, fursa ni yake Tom Fletcher, Mratibu wa Umoja wa mataifa wa Misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura akihitimisha ziara yake Goma Mashariki mwa DRC amezungumza na waandishi wa habari akieleza kuwa raia wameteseka vya kutosha na ukata unawazidishia madhila”Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Duration:00:09:59

Ask host to enable sharing for playback control

WHO yasema vifaa vya matibabu vimeingia Gaza lakini bado havitoshi

6/27/2025
Hatimaye shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni, WHO limeweza kufikisha huko Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli, shehena ya kwanza ya vifaa vya matibabu ikiwa ni mara ya kwanza tangu tarehe pili mwezi Machi mwaka huu. Anold Kayanda na maelezo zaidi.

Duration:00:02:01

Ask host to enable sharing for playback control

Jifunze Kiswahili: Maana ya neno AFRITI KIJITI

6/26/2025
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili mchambuzi wetu mlumbi wa Kiswahili Joramu Nkumbi kutoka nchini Tanzania, anafafanua maana ya neno "AFRITI KIJITI.”

Duration:00:00:35

Ask host to enable sharing for playback control

26 JUNI 2025

6/26/2025
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania, ambako mshikamano na wakimbizi unatekelezwa kwa vitendo na mashirika ya Umoja Mataifa likiwemo lile la Chakula na Kilimo (FAO) na la kuhudumia wakimbizi, UNHCR kupitia Programu wa Pamoja ya Kigoma (KJP).Katika siku ya kimataifa ya kupambana na dawa za kulevya na usafirishaji haramu, ripoti mpya ya dunia ya Dawa za Kulevya mwaka 2025 iliyotolewa leo imeonya kuwa kutokuwepo kwa utulivu duniani kunachochea ongezeko la matumizi ya dawa za kulevya na uhalifu wa kupangwa. Kwa mujibu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Dawa na Uhalifu UNODC, watu milioni 316 walitumia mihadarati mwaka 2023. Mkurugenzi Mtendaji wa UNODC, Ghada Waly, amesema "Makundi haramu yanatumia migogoro kama fursa tunahitaji ushirikiano na uwekezaji kulinda jamii zetu.”Leo ni kumbukizi ya uzinduzi wa Chata ya Umoja wa Mataifa miaka 80 iliyopita mjini San Francisco, hatua iliyoweka msingi wa kuundwa kwa Umoja wa Mataifa mnamo Oktoba 24, 1945. Katibu Mkuu António Guterres anasema Umoja wa Mataifa bado unaakisi matumaini yaliyozaliwa kutoka kwenye majivu ya vita naye mwanahistoria Stephen Schlesinger akizungumza na UN News ameakumbusha kuwa “Chata hii ilikuwa kilio cha wanadamu wakitafuta amani, suluhu za mazungumzo, na maisha bora duniani.”Asilimia 93 ya kaya Gaza hazina uhakika wa maji safi kutokana na ukosefu wa mafuta unaopelekea mifumo ya maji kukaribia kusambaratika yameonya mashirika ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa leo yakiongeza kuwa familia zinakumbwa na njaa kali, wakila mlo mmoja kwa siku huku watu wazima wakikosa kula ili kuwasaidia watoto na wazee.Na leo katika kujifunza lugha ya Kiswahili mchambuzi wetu mlumbi wa Kiswahili Joramu Nkumbi kutoka nchini Tanzania, anafafanua maana ya neno "AFRITI KIJITI”Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Duration:00:10:13

Ask host to enable sharing for playback control

UN80: Umoja wa Mataifa wajitathmini kwa ajili ya karne mpya

6/25/2025
Katika dunia inayokumbwa na migogoro inayoendelea kuongezeka, kupanuka kwa pengo la usawa, na kupungua kwa imani katika taasisi za kimataifa, Umoja wa Mataifa umeanzisha juhudi kabambe za kuboresha namna unavyowahudumia watu kote ulimwenguni. Mpango wa UN80, uliotangazwa mwezi Machi na Katibu Mkuu António Guterres, ni juhudi ya mfumo mzima inayolenga kurahisisha utendaji kazi, kuongeza ufanisi, na kuthibitisha tena umuhimu wa Umoja wa Mataifa katika dunia inayobadilika kwa kasi. Je nini nini kinatarajiwa katika mpango huo wa UN80? Ungana na Flora Nducha katika Makala hii

Duration:00:03:02

Ask host to enable sharing for playback control

Wanawake wa Somalia na usafirishaji baharini

6/25/2025
Nchini Somalia, suala la usawa wa kijinsia katika sekta ya baharini limepatiwa kipaumbele kwenye mjadala kuhusu wanawake katika tasnia hiyo, mjadala uliofanyika kwenye mji mkuu Mogadishu ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mabaharia inayoadhimishwa tarehe 25 mwezi Juni kila mwaka ikibeba maudhui Meli yangu isiyo na unyanyasaji. Sharon Jebichii anatupasha zaidi.

Duration:00:02:22

Ask host to enable sharing for playback control

Upatikanaji wa nishati duniani umeboreka lakini uwezeshaji kifedha bado unahitajika kupunguza tofauti – Ripoti ya UN

6/25/2025
Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa inayofuatilia maendeleo kuelekea kutimiza Lengo la Umoja wa Mataifa la Maendeleo Endelevu namba 7 (SDG 7) linaloangazia nafasi muhimu ya nishati mbadala imetoa wito wa ufadhili zaidi kwani ingawa asilimia 92 ya watu duniani sasa wanapata umeme, lakini watu milioni 666 wengi wao wakiwa Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara bado hawapati umeme. Anold Kayanda na maelezo zaidi.

Duration:00:02:16

Ask host to enable sharing for playback control

25 JUNI 2025

6/25/2025
Hii leo Jarida linamulika ripoti ya nishati jadidifu duniani, Afrika ikiwa bado inasuasua; Harakati za mabaharia wanawake Somalia, Mpango wa Umoja wa Mataifa wa UN80 na baba na malezi ya mtoto nchini Tanzania.Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa inayofuatilia maendeleo kuelekea kutimiza Lengo la Umoja wa Mataifa la Maendeleo Endelevu namba 7 (SDG 7) linaloangazia nafasi muhimu ya nishati mbadala imetoa wito wa ufadhili zaidi kwani ingawa asilimia 92 ya watu duniani sasa wanapata umeme, lakini watu milioni 666 wengi wao wakiwa Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara bado hawapati umeme. Anold Kayanda na maelezo zaidi.Nchini Somalia, suala la usawa wa kijinsia katika sekta ya baharini limepatiwa kipaumbele kwenye mjadala kuhusu wanawake katika tasnia hiyo, mjadala uliofanyika kwenye mji mkuu Mogadishu ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mabaharia inayoadhimishwa tarehe 25 mwezi Juni kila mwaka ikibeba maudhui Meli yangu isiyo na unyanyasaji. Sharon Jebichii anatupasha zaidi.Je wafahamu kuhusu UN80? Flora Nducha anadadavua kwenye makala.Mashinani: Aloyce Siame, baba wa mtoto mwenye umri wa miaka 12 kutoka Tanzania ambaye kupitia Mpango wa Vijana uitwayo “Furaha”, unaoungwa mkono na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF na wadau wake sasa ni mmoja wa wanaume wanaojitokeza kwa malezi ya watoto na familia zao.

Duration:00:10:30

Ask host to enable sharing for playback control

24 JUNI 2025

6/24/2025
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina nayomulika mabaharia wanawake, ambapo tunamsikia mmoja wao, Mary Jane Siy Chuan, Fundi wa Umeme melini, akisema, “ninapoingia melini, wafanyakazi wengine wanahoji kama vile, kwa nini kuna mwanamke baharini.”Kukiwa na dalili za kuwa sitisho la mapigano kati ya Iran na Israel linaanza kushika mizizi, mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki, IAEA Rafael Grossi. ametoa wito kwa Iran kuanza tena ushirikiano na jumuiya ya kimataifa ili kupunguza mvutano unaoendelea kuhusu mpango wake wa nyuklia. Grossi amesema amempa Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, ombi la kukutana na kushirikiana, “akitilia mkazo kuwa hatua hii inaweza kufungua njia ya suluhisho la kidiplomasia kwa mgogoro wa muda mrefu” kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran.Msemaji wa Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa (OHCHR) Thameen Al-Kheetan ameripoti leo kwamba hadi kufikia sasa takribani Wapalestina 410 wameuawa na jeshi la Israeli wakati wakijaribu kupata msaada kutoka kwa vituo vipya vya misaada vilivyokumbwa na utata huko Gaza.Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, limeripoti leo kuwa linakadiria kuwa wakimbizi milioni 2.5 duniani kote watahitaji kuhamishiwa Kwenda katika nchi nyingine mwaka ujao.Na mashianani fursa ni yake Zahra Nader, raia wa Afghanistan ambaye ni mwandishi wa habari na mwanaharakati wa haki za wanawake, anayeishi uhamishoni kutokana na zahma nchini mwake. Akizungumza kutoka Geneva, USwisi anasimulia hali halisi ya wanawake nchini Afghanistan, huku akisisitiza umuhimu wa kuzingatia haki zao..Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!

Duration:00:09:58

Ask host to enable sharing for playback control

TANLAP Tanzania tunahamasisha wanawake wengi kushiriki kwenye uchaguzi ili washiriki kuamua mambo yanayowahusu - Christina Kamili Ruhinda

6/23/2025
Katika mahojiano haya, Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Mashirika yanayotoa huduma ya msaada wa kisheria nchini Tanzania, TANLAP, Christina Kamili Ruhinda alipozungumza na Anold Kayanda wa Idhaa hii kandoni mwa Mkutano wa Kamisheni ya hali ya wanawake duniani CSW69 uliofanyika mapema mwaka huu hapa New York, Marekani, anaeleza wanavyotekeleza mpango wao wa kuhakikisha wanawake wanapata nafasi zaidi kwenye meza za uamuzi nchini Tanzania.

Duration:00:03:13

Ask host to enable sharing for playback control

Muziki waunganisha jamii zilizogawanyika Malakal nchini Sudan Kusini

6/23/2025
Katika juhudi za kuimarisha mshikamano na kurejesha matumaini miongoni mwa jamii zilizotengana kwa migogoro, ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini, UNMISS, kwa kushirikiana na shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, hivi karibuni waliandaa tamasha maalum la muziki katika mji wa Malakal, jimbo la Upper Nile – eneo ambalo kwa miezi ya hivi karibuni limekuwa kitovu cha machafuko. Sharon Jebichii anatupasha zaidi

Duration:00:02:05

Ask host to enable sharing for playback control

23 JUNI 2025

6/23/2025
Hii leo jaridani tunaangazia mashambulizi ya anga yaliyofanywa na Marekani dhidi ya vituo vya nyuklia vya Iran, na juhudi za kurejesha matumaini miongoni mwa jamii zilizotengana kwa migogoro Sudan Kusini. Makala tunakwenda nchini Tanzania na mashinani nchini Kenya.Hali ya taharuki yaendelea kushuhudiwa Mashariki ya Kati kufuatia mashambulizi ya anga yaliyofanywa na Marekani dhidi ya vituo vya nyuklia vya Iran mwishoni mwa wiki. Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki IAEA, Rafael Grossi, leo ametoa wito wa dharura wa shirika hilo kuruhusiwa kufika kwenye maeneo hayo yaliyoharibiwa, ili kutathmini kiwango halisi cha uharibifu.Katika juhudi za kuimarisha mshikamano na kurejesha matumaini miongoni mwa jamii zilizotengana kwa migogoro, ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini, UNMISS, kwa kushirikiana na shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, hivi karibuni waliandaa tamasha maalum la muziki katika mji wa Malakal, jimbo la Upper Nile – eneo ambalo kwa miezi ya hivi karibuni limekuwa kitovu cha machafuko.Katika makala Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Mashirika yanayotoa huduma ya msaada wa kisheria nchini Tanzania, TANLAP, Christina Kamili Ruhinda anaeleza wanavyotekeleza mpango wao wa kuhakikisha wanawake wanapata nafasi zaidi kwenye meza za uamuzi nchini Tanzania.Na mashianani fursa ni yake Priscillah Lesurkukwa, Mwanamke mkulima kutoka kaunti kame ya Samburu nchini Kenya ambaye ni mnufaika wa mradi wa Shrika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula WFP, ambao umewapatia wakulima mafunzo ya kutengeneza makinga maji na kuchimba mashimo yenye umbo la nusu mwezi ili kuvuna na kuhifadhi maji kwenye mashamba yao, na sasa mbinu hizo zimebadilisha mazingira kuwa na malisho ya kijani kibichi na miti inayostawi.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Duration:00:10:27

Ask host to enable sharing for playback control

Baada ya Marekani kushambulia vito vya nyuklia vya Iran, IAEA yataka fursa kutathimini uharibifu

6/23/2025
Hali ya taharuki yaendelea kushuhudiwa Mashariki ya Kati kufuatia mashambulizi ya anga yaliyofanywa na Marekani dhidi ya vituo vya nyuklia vya Iran mwishoni mwa wiki. Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki IAEA, Rafael Grossi, leo ametoa wito wa dharura wa shirika hilo kuruhusiwa kufika kwenye maeneo hayo yaliyoharibiwa, ili kutathmini kiwango halisi cha uharibifu. Flora Nducha na tarifa zaidi

Duration:00:01:56

Ask host to enable sharing for playback control

Burundi yamwezesha mkimbizi fundi seremala kutoka DRC kuendeleza stadi yake na kujipatia kipato

6/20/2025
Burundi inaonesha kwa vitendo mshikamano na wakimbizi kwa kuwapa fursa ya kupata elimu, huduma za afya, ajira na huduma nyingine za kitaifa, na hivyo kuwasaidia kuchangia katika jamii wanamoishi. Miongoni mwa wakimbizi hao ni Amani Lukoo Elie kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC akiambana na mke wake na watoto 5 wamesaka hifadhi kusini-magharibi baada ya kukimbia mapigano jimboni Kivu Kaskazini. Kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, Assumpta Massoi amefuatilia kile wanachofanya sasa ili kuweza kujikimu.

Duration:00:03:21

Ask host to enable sharing for playback control

UN: Mshikamano na wakimbizi uwe kwa vitendo na si maneno matupu

6/20/2025
Leo ni Siku ya Wakimbizi Duniani, mwaka huu ikibeba maudhui “Mshinamano na wakimbizi” na Umoja wa Mataifa umetaka mshikamano huo kwa vitendo wakati idadi ya watu wanaolazimika kufungasha virago na kukimbia makayo yao ikifikia kiwango cha kihistoria. Flora Nducha na taarifa zaidi

Duration:00:01:45

Ask host to enable sharing for playback control

20 JUNI 2025

6/20/2025
Hii leo jaridani tunaangazia siku ya Wakimbizi Duniani, mwaka huu ikibeba maudhui “Mshinamano na wakimbizi”, tukisikia ujumbe wa Umoja wa Mataifa na kazi wanazozifanya kuinua Maisha ya wakimbizi, na pia tunakuletea sauti za wakimbizi kutoka DRC, Burundi, Ethiopia na Sudan Kusini.Leo ni Siku ya Wakimbizi Duniani, mwaka huu ikibeba maudhui “Mshinamano na wakimbizi” na Umoja wa Mataifa umetaka mshikamano huo kwa vitendo wakati idadi ya watu wanaolazimika kufungasha virago na kukimbia makayo yao ikifikia kiwango cha kihistoria.Tukisalia na siku ya wakimbizi duniani tunaelekea eneo la Mata, karibu na mpaka wa Ethiopia na Sudan Kusini, ambakomaelfu ya wakimbizi kutoka Sudan Kusini wanapokea msaada wa dharura kupitia juhudi za Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, WFP. unaolenga kuwalinda baada ya kukimbia mapigano makali nchini mwao. Nyibol Chueny Puok, mama wa watoto 4 ni miongoni mwao.Katika makala Assumpta Massoi kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR anakupeleka Kusini-Magharibi mwa Burundi kwenye kituo cha wakimbizi cha Musenyi kumsikia mkimbizi kutoka DRC ambaye ananufaika na kauli mbiu ya siku ya wakimbizi mwaka huu ya Mshikamano na Wakimbizi.Na mashianani tukisalia na siku ya wakimbizi duniani, tutakwenda nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC kumsikia mtoto mkimbizi ambaye alitumikishwa katika vita na waasi wenye silaha.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Duration:00:09:58

Ask host to enable sharing for playback control

Wakimbizi kutoka Sudan Kusini wanapatiwa msaada na WFP mpakani mwa Ethiopia

6/20/2025
Katika eneo la Mata, karibu na mpaka wa Ethiopia na Sudan Kusini, ambakomaelfu ya wakimbizi kutoka Sudan Kusini wanapokea msaada wa dharura kupitia juhudi za Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, WFP. unaolenga kuwalinda baada ya kukimbia mapigano makali nchini mwao. Nyibol Chueny Puok, mama wa watoto 4 ni miongoni mwao. Sharon Jebichi anatupasha zaidi...

Duration:00:02:04

Ask host to enable sharing for playback control

Jifunze Kiswahili: Maana ya neno KIHORO

6/19/2025
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "KIHORO!"

Duration:00:00:40