Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
United Nations
Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Location:
New Rochelle, NY
Genres:
News & Politics Podcasts
Networks:
United Nations
Description:
Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Twitter:
@HabarizaUN
Language:
Swahili
Contact:
9178215291
Episodes
Nilikuwa miongoni mwa Wacuba wa kwanza kujifunza Kiswahili: Profesa Jacomino
12/27/2024
Ujumuishwasji wa lugha mbalimbali katika dunia iliyoshikamana katika Nyanja mbalimbali ni moja ya malengu ya Umoja wa Mataifa kuanzia katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa hadi kwenye nchi wanachama unalichagiza hilo. Hamasa hiyo imezichagiza nchi nyingi kuanza kukumbatia lugha ambazo kwa asili hazizungumzwi kama alivyobaini Flora Nducha wa Idhaa hii ambaye hivi karibuni alikuwa Cuba kwenye Kongamano la Kimataifa la Kiswahili na kukutana na Profesa Juan Jacomino ambaye ni mhadhiri katika chuo kikuu cha Havana na ni miongoni mwa watu wa mwanzo waliokwenda Tanzania kujifunza Kiswahili na sasa anakifundisha nchini mwake Cuba. Anafafanua kuhusu safari yake ya kujua Kiswahili katika makala hii..
Duration:00:05:03
Siku ya Kimataifa ya Kujitayarisha dhidi ya magonjwa ya mlipuko, Mkuu wa Umoja wa Mataifa atoa wito
12/27/2024
Katika kuandhimisha Siku ya Kimataifa ya Kujitayarisha dhidi ya Magonjwa ya Mlipuko, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametoa wito kwa nchi kote ulimwenguni kuzingatia masomo yaliyopatikana katika dharura za kiafya zilizopita ili kusaidia kujiandaa kwa dharura zijayo. Assumpta Massoi anaeleza zaidi.
Duration:00:01:32
27 DESEMBA 2024
12/27/2024
Hii leo jaridani tunaangazia sherehe za krismasi katika ukanda wa Gaza lich ya migogoro inayoendelea, na magonjwa ya mlipuko. Makala inatupeleka Havana Cuba na mashinani nchini Uganda, kulikoni?Katika kuandhimisha Siku ya Kimataifa ya Kujitayarisha dhidi ya Magonjwa ya Mlipuko, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametoa wito kwa nchi kote ulimwenguni kuzingatia masomo yaliyopatikana katika dharura za kiafya zilizopita ili kusaidia kujiandaa kwa dharura zijayo.Tukiwa bado katika msimu wa sikukuu ya krismasi, tunakwenda mji wa Gaza, huko Ukanda wa Gaza, Mashariki ya Kati kusikia jinsi sikukuu hii ilivyoadhimishwa na hisia mchanganyiko kwenye kanisa katoliki la Familia Takatifu kwenye viunga vya zamani kwenye mji huo.Makala inatupeleka Havana Cuba kuangazia umuhimu wa utekelezaji wa moja ya ajenda za Umoja wa Mataifa ya kukumbatia lugha mbalimbali duniani ambapo Flora Nducha wa Idhaa hii akiwa Cuba hivi karibuni kwenye kongamano la Kimataifa la Kiswalihi alikutana na raia wa nchi ambaye ni mwalimu wa Kiswahili.Mashinani fursa ni yake Ange Rukenura, msichana alieyekimbia makazi yake pamoja na ndugu zake sita kufuatia mashambulizi ya waasi waliojihami nchini Jamhuri ya Kidemocrasi ya Congo, DRC akisema licha ya rasilimali ndogo anashukuru ukarimu wa Uganda na msaada wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR kwa kuwapatia matumaini.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Duration:00:09:57
Sherehe za Krismasi katika ukanda wa Gaza, wakimbizi wa ndani wataka vita vikome
12/27/2024
Tukiwa bado katika msimu wa sikukuu ya krismasi, tunakwenda mji wa Gaza, huko Ukanda wa Gaza, Mashariki ya Kati kusikia jinsi sikukuu hii ilivyoadhimishwa na hisia mchanganyiko kwenye kanisa katoliki la Familia Takatifu kwenye viunga vya zamani kwenye mji huo. Assumpta Massoi na taarifa zaidi.
Duration:00:02:03
24 DESEMBA 2024
12/24/2024
Hii leo jaridani tunakuletea mad akwa kina inayotupeleka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kumulika harakati za kusaidia manusura wa ukatili wa kingono na kijinsia kwenye mizozo. Pia tunakuletea muhtasari wa había za Sudan, Uganda na Tanzania, Mashinani tunarejea Sudan.Ripoti ya Kamati ya Tathmini ya Viwango vya Njaa (IPC) iliyotolewa leo inaeleza kwamba imegundua kuwa kuna maeneo matano zaidi nchini Sudan ambayo yanakabiliwa na baa la njaa kati ya mwezi huu wa Desemba na Mei mwaka ujao wa 2025. Ripoti hiyo imeyataja maeneo hayo kuwa ni ya Darfur Kaskazini yaani Um Kadadah, Melit, El Fasher, Twawisha, na Al Lait.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limekaribisha mchango wa EURO milioni 1 kutoka serikali ya Ujerumani ili kusaidia shughuli za lishe na ustawi kwa zaidi ya wakimbizi na wasaka hifadhi 254,000 nchini Uganda ambayo inawahifadhi wakimbizi milioni 1.7.Na Kikosi cha 7 cha Walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania, TANBAT 7 kilichokuwa kinahudumu katika Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kuleta Utulivu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR (MINUSCA) kimerejea nyumbani Tanzania kikijivunia kuwa kikosi cha kwanza cha nchi hiyo kupokea barua ya pongezi kutoka Umoja wa Mataifa.Mashinani fursa ni yake Najwa Mohamed, mama mjamzito kutoka Jabal Moya nchini Sudan ambaye amepoteza makazi yake kufuatia vurugu zinazoendelea nchini humo na kulieleza Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya uzazi, UNFPA kwamba hali ni ngumu hasa kwa wanawake wajawazito.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Duration:00:12:51
Mradi wa kilimo cha umwagiliaji warejesha matumaini kwa wakulima wa Masvingo, Zimbabwe
12/23/2024
Hivi karibuni mkutano wa Umoja wa Mataifa wa kuzuia kuenea kwa jangwa, ulikunja jamvi huko Riyadh, Saudi Arabia ambapo Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Kilimo, IFAD ulitumia fursa hiyo kuelezea harakati zake za kusaidia wakulima barani Afrika walioathiriwa vibaya na kuenea kwa jangwa. Miongoni mwa mataifa hayo ni Zimbabwe ambako IFAD imeshaanza kuchukua hatua na kuleta nuru kwa wakulima kama anavyosimulia Assumpta Massoi kwenye makala hii.
Duration:00:03:09
Mkuu wa ofisi ya OCHA Tom Fletcher aeleza aliyoyashuhudia ziara yake ya kwanza Mashariki ya Kati
12/23/2024
Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Dharura, OCHA, Tom Fletcher akihitimisha ziara yake ya kwanza katika eneo la Mashariki ya kati tangu hivi karibuni alipochukua wadhifa huo ameeleza kuwa alichokishuhudia katika ukanda huo ni hali tete. Selina Jerobon anaeleza zaidi.
Duration:00:01:56
23 DESEMBA 2024
12/23/2024
Hii leo jaridani tunaangazia ziara ya Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Dharura, OCHA, Tom Fletcher mashariki wa kati, na uwezeshaji wa vijana katika sekta ya kilimo nchini humo. Makala inatupeleka nchini Zimbabwe na mashinani nchini Kenya, kulikoni?Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Dharura, OCHA, Tom Fletcher akihitimisha ziara yake ya kwanza katika eneo la Mashariki ya kati tangu hivi karibuni alipochukua wadhifa huo ameeleza kuwa alichokishuhudia katika ukanda huo ni hali tete.Mradi wa pamoja wa shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO ujulikanao kama Nabta kwa lugha ya Kiarabu ukimaanisha "mche" ambao lengo lake ni kuwasaidia vijana wajasiriamali kubadili mawazo yao kuwa biashara ya kilimo yenye mafanikio umeleta nuru kwa Alaa Khattab kijana aliyekuwa na ndoto ya kuwa mfanyabiashara wa kilimo nchini Syria.Katika makala Assumpta Massoi anakupeleka Zimbabwe kumulika nuru iliyofikia wakulima baada ya Umoja wa Mataifa kuona jinsi mabadiliko ya tabianchi yalivyoathiri shughuli za kilimo.Mashinani fursa ni yake Rukia, kijana wa kike kutoka Tana River nchini Kenya ambaye kupitia mafunzo na uwezeshaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM, yeye hasiti kutoa tahadhari za mapema na kuwahamasisha jamii kujiepusha na madhara panapotokea majanga ya mabadiliko ya tabianchi.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Duration:00:10:00
Hadithi ya Alaa Khattab: Kutoka kuwa mzalishaji mdogo kijijini kwake hadi kuwa msafirishaji wa Kikanda wa achari
12/23/2024
Mradi wa pamoja wa shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO ujulikanao kama Nabta kwa lugha ya Kiarabu ukimaanisha "mche" ambao lengo lake ni kuwasaidia vijana wajasiriamali kubadili mawazo yao kuwa biashara ya kilimo yenye mafanikio umeleta nuru kwa Alaa Khattab kijana aliyekuwa na ndoto ya kuwa mfanyabiashara wa kilimo nchini Syria. Flora Nducha anatujuza zaidI.
Duration:00:02:09
Wasichana wakipewa fursa hakuna mchezo utakaowashinda: Saido Noor
12/20/2024
Kutana na Saido Omar Noor, binti mwenye umri wa miaka 25 mkimbizi kutoka Somalia anayeishi Kakuma kambi kubwa zaidi ya wakimbizi nchini Kenya. Kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR anasema katika jamii yake ni yeye mwanamke pekee wa Kisomali anayecheza mpira kwa kikapu au basketball. Flora Nducha na taarifa zaidi..
Duration:00:03:31
Rwanda yatangaza mwisho wa mlipuko wa Marburg, WHO yapongeza Rwanda
12/20/2024
Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) limeipongeza serikali ya Rwanda kwa kufanikiwa kuudhibiti mlipuko wa ugonjwa wa Maburg. Hii leo Rwanda imetangaza mwisho wa mlipuko wa hivi karibuni wa ugonjwa huo baada ya kutokuwepo maambukizi mapya katika siku 42 na mgonjwa wa mwisho akiwa amepimwa mara mbili bila kukutwa na ugonjwa kama matakwa ya WHO yanavyotaka ili kutangaza kuisha kwa mlipuko wa magonjwa namna hii. Selina Jerobon na maelezo zaidi.
Duration:00:02:03
20 DESEMBA 2024
12/20/2024
Hii leo jaridani tunaangazia jitihada za kuudhibiti mlipuko wa ugonjwa wa Maburg nchini Rwanda, na juhudi za kuchunguza virusi vya VVU nchini Ghana. Makala tunakupeleka nchini Kenya na mashinani nchini DRC, kulikoni?Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) limeipongeza serikali ya Rwanda kwa kufanikiwa kuudhibiti mlipuko wa ugonjwa wa Maburg. Hii leo Rwanda imetangaza mwisho wa mlipuko wa hivi karibuni wa ugonjwa huo baada ya kutokuwepo maambukizi mapya katika siku 42 na mgonjwa wa mwisho akiwa amepimwa mara mbili bila kukutwa na ugonjwa kama matakwa ya WHO yanavyotaka ili kutangaza kuisha kwa mlipuko wa magonjwa namna hii.Mwaka 2020 Ghana iliripoti kuwa na watu 350,000 wanaioshi na virusi vya Ukimwi na kati yao hao 31,000 walikuwa ni wajawazito. Jambo lililoshtua ni kwamba ni sehemu ndogo mno ya wajawazito hao ndio walipimwa kufahamu iwapo wana VVU au la. Jambo lililofanya serikali kwa kushirikiana na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF kuchukua hatua.Makala inatupeleka kwenye kambi ya wakimbizi ya Kakuma iliyokoko Kaunti ya Turkana Kaskazini Magharibi mwa Kenya kukukutanisha na mkimbizi kutoka Somalia anayetumia mpira wa kikapu anatumia mpira wa vikapu kuhamasisha jamii yake na kupinga mil ana desturi zisizofaa.Mashinani ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Mpira wa Kikapu, fursa ni yake Danny Batachoka, mwanariadha wa Paralimpiki kutoka Goma nchini Jamhuri ya kidemocrasia ya Congo, DRC ambaye kupitia video ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo MONUSCO, anasema ana ndoto ya kuwa mmoja wa wachezaji wakubwa wa mpira wa vikapu katika kitengo chake.” Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Duration:00:10:53
Kipimo cha GeneXpert chaleta mapinduzi kwenye upimaji wa VVU nchini Ghana
12/20/2024
Mwaka 2020 Ghana iliripoti kuwa na watu 350,000 wanaioshi na virusi vya Ukimwi na kati yao hao 31,000 walikuwa ni wajawazito. Jambo lililoshtua ni kwamba ni sehemu ndogo mno ya wajawazito hao ndio walipimwa kufahamu iwapo wana VVU au la. Jambo lililofanya serikali kwa kushirikiana na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF kuchukua hatua. Ripoti ya Assumpta Massoi inafafanua zaidi.
Duration:00:02:00
Jifunze Kiswahili: Ufafanuzi wa neno Akraba
12/19/2024
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo mchambuzi wetu mlumbi wa Kiswahili Joramu Nkumbi kutoka nchini Tanzania, anafafanua maana ya neno “AKRABA.”
Duration:00:00:38
19 DESEMBA 2024
12/19/2024
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Syria, ambako viongozi wa ngazi mbalimbali za Umoja wa Mataifa wamendelea kusisitiza hitaji la kutanguliza ulinzi wa manusura na uhifadhi wa ushahidi wa uhalifu. Pia tunapata ufafanuzi wa neno na muhtasari wa habari.Karla Quintana kutoka Mexico ameteuliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres hii leo kuongoza Taasisi Huru ya kuchunguza watu waliotoweshwa nchini Syria, taasisi ambayo imeundwa na Baraza la Kuu la Umoja wa Mataifa mwezi Juni mwaka jana 2023. Guterres amewaambia waandishi wa habari hii leo kwamba yeye na timu yake lazima waruhusiwe kutekeleza kwa kina jukumu lao, na vile vile mifumo yote ya kimataifa ya kusongesha ulinzi wa haki za binadamu nchini Syria na uwajibikaji wa uhalifu uliotendwa lazima wawe na wanachohitaji ili kutekeleza majukumu yao muhimu.Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekuwa na kikao cha ngazi ya mawaziri kuhusu Akili Mnemba, au AI ambapo Katibu Mkuu António Guterres amesema pamoja faida kubwa ya teknolojia hiyo bado kuna changamoto iwapo haitasimamiwa vema na binadamu. Hivyo amependekeza kuundwa mwa mfumo wa kimataifa wa kuendeleza Akili Mnemba kwa uwiano na usawa, ukijikita kusaidia nchi zinazoendelea kuzuia kuibuka kwa pengo la teknolojia hiyo kati ya walio nayo na wasio nayo.Na huko Bunia, jimboni Ituri mashariki mwa Jamhuri ya Kidemorkrasia ya Congo, DRC vijana 24 wakiwemo wanawake 6 wamenufaika na mafunzo ya siku tano ya mbinu za kisasa za kilimo kutoka walinda amani wa Bangladeshi wanaohudumu kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo MONUSCO. Lengo ni kuwezesha kilimo kuwa chanzo cha kipato kwa wakazi na kuimarisha uchumi wa eneo hilo.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo mchambuzi wetu mlumbi wa Kiswahili Joramu Nkumbi kutoka nchini Tanzania, anafafanua maana ya neno “AKRABA.” Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Duration:00:09:43
FAO Tanzania yatoa mafunzo ya ufugaji wa nyuki kwa wenyeji Tanzania kupitia Mradi wa ACP MEAs 3
12/18/2024
Mradi wa ACP MEAs 3 unaoendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO, na kufadhiliwa na Muungano wa Ulaya, EU umetoa mafunzo ya ufugaji nyuki kwa wakulima nchini Tanzania. Mradi huu unawapa wakulima zana na ujuzi muhimu katika ufugaji nyuki endelevu, na hivyo kuboresha maisha yao huku wakikuza bayoanuwai na uhifadhi wa mazingira. Kwa kuunga mkono jamii za wenyeji, Mradi huu unalenga kukuza ukuaji wa uchumi na kuwawezesha wakulima kulinda wachavushaji, ambao ni muhimu kwa uzalishaji katika kilimo na afya ya mfumo ikolojia. Tupate simulizi zaidi katika makala hii iliyoandaliwa na Flora Nducha kupitia video ya FAO Tanzania.
Duration:00:02:50
Guterres: Siku ya Kimataifa ya Wahamiaji tujikumbushe changamoto wanazokumbana nazo
12/18/2024
Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya Uhamiaji, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kupitia ujumbe wake mahususi kwa ajili ya Siku ya Kimataifa ya Wahamiaji ametoa wito kwa ulimwengu kuitumia siku hii kujikumbusha kwamba pamoja na kwamba tunasherehekea michango ambayo mamilioni ya wahamiaji hutoa kwa jamii leo pia ni siku ya kujikumbusha changamoto ambazo wahamiaji wanaweza kukumbana nazo. Selina Jerobon na maelezo zaidi.
Duration:00:01:42
18 DESEMBA 2024
12/18/2024
Hii leo jaridani tunaangazia siku ya wahamiaji duniani ikimulika mchango wa wakimbizi na wahamiaji katika ukuaji wa kiuchumi na kukuza jamii zao n aza wenyeji. Tutasikia kutoka mkuu wa IOM, Katibu Mkuu wa UN na wahamiaji Burundi na Chad. Pia tunaangazia ufugaji nyuki Tanzania.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kupitia ujumbe wake mahususi kwa ajili ya Siku ya Kimataifa ya Wahamiaji ametoa wito kwa ulimwengu kuitumia siku hii kujikumbusha kwamba pamoja na kwamba tunasherehekea michango ambayo mamilioni ya wahamiaji hutoa kwa jamii leo pia ni siku ya kujikumbusha changamoto ambazo wahamiaji wanaweza kukumbana nazo.Nimefurahi sana kwani binti yangu mwenye ulemavu ambaye tulihamia naye makazi ya muda kufuatia kuongezeka kina cha maji ya Ziwa Tanganyika, hapa Burundi sasa amepatiwa stadi za kumwezesha kujikwamua kiuchumi. Ni kauli ya Odette Niyonkuru, raia mhamiaji wa ndani nchini Burundi akizungumzia mustakabali wa binti yake huyo kwenye video ya shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji, IOM.Makala inatupeleka nchini Tanzania kufuatilia Mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO uitwao ACP MEAs 3 ambao umwewapa wakulima zana na ujuzi muhimu katika ufugaji nyuki endelevu kwa lengo la kuboresha maisha yao huku wakikuza bayoanuwai na uhifadhi wa mazingira. Kupitia video iliyoandaliwa na FAO Tanzania Selina Jerobon amefuatilia mafanikio ya mradi huu na kituandalia makala hii.Na mashinani katika siku hii ya kimataifa ya wahamajia Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji, IOM linasisitiza umuhimu wa kuwawezesha wanawake na wasichana walio ukimbizini na kuongeza mikakati ya kifedha inayozingatia jinsia. Bi Banti Ahmat ni mmoja wa wakimbizi na anelezea jinsi ambavyo mradi wa IOM wa bustani za jamii unavyoleta matokeo chanya kwa wahamiaji na jamii za wenyeji nchini Chad.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Duration:00:09:54
Mafunzo ya IOM kwa msichana mhamiaji mwenye ulemavu, yaleta furaha kwa mama yake
12/18/2024
Nimefurahi sana kwani binti yangu mwenye ulemavu ambaye tulihamia naye makazi ya muda kufuatia kuongezeka kina cha maji ya Ziwa Tanganyika, hapa Burundi sasa amepatiwa stadi za kumwezesha kujikwamua kiuchumi. Ni kauli ya Odette Niyonkuru, raia mhamiaji wa ndani nchini Burundi akizungumzia mustakabali wa binti yake huyo kwenye video ya shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji, IOM. Odette anaenelea kueleza manufaa ya uwezeshaji huu kwa bintiye kama anavyofuatilia Assumpta Massoi.
Duration:00:02:13
17 DESEMBA 2024
12/17/2024
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika mafanikio katika kuzuia maambukizi mapya ya VVU na juhudi za vijana wakimbizi nchini Uganda kuhakikisha hilo. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani inayotupeleka Gaza.Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Syria Geir O. Pedersen bado yuko nchini Syria alikowasili jana Jumapili ikiwa ni wiki moja baada ya wapiganaji wa Hayʼat Tahrir al-Sham (HTS) walioko kwenye orodha ya vikundi vya kigaidi kutwaa mji mkuu Damascus na kusababisha Rais Bashar Al-Assad kukimbia nchi.Mwaka 2024 ukielekea ukingoni, sirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR nchini Uganda limetoa rai kwa jumiya ya kimataifa kutolisahau taifa hilo la Afrika Mashariki ambalo ni maskani ya idadi kubwa zaidi ya waomba hifadhi na wakimbizi barani Afrika. Rai hiyo iliyotolewamwishoni mwa wiki inataka ufadhili wa fedha uongezwe ili liweze kuendelea kukirimu watu hao ambao wengi wanakimbia machafuko.Katika makala Assumpta Massoi anakupeleka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na Ethiopia kumulika mwelekeo wa usajili wa watoto wanapozaliwa na faida zake. Na mashinani Maram, mama kutoka Deir al-Balah Gaza, ambako familia zinahaha kuokoa mali zao na kukarabati mahema yao yaliyoharibiwa na upepo mkali na maji ya mvua wakati huu wa msimu wa baridi, na kuleta athari kwa watoto wao.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Duration:00:10:48