Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu-logo

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

United Nations

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Location:

New Rochelle, NY

Description:

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Twitter:

@HabarizaUN

Language:

Swahili

Contact:

9178215291


Episodes
Ask host to enable sharing for playback control

Vijana tuna jukumu muhimu katika maendeleo ya jamii zetu tuchangamkie fursa: Winfred Njiru

4/11/2025
Umoja wa Mataifa unaendelea kuchagiza vijana kujitokeza na kushiriki katika kusongesha ajenda ya maendeleo endelevu katika jamii zao na ndio maana wiki iliyopita majadiliano ya viongozi wastaafu kuhusu maendeleo endelevu ya Club De Madrid yaliyofanyika Nairobi Kenya yalitoa fursa kwa vijana kupaza sauti zao kuhusu jinsi wataavyochangia kufanikisha malengo hayo. Winfred Njiru mwanafunzi wa chuo kikuu fani ya uhakiki au quantity surveyor alizungumza na Stella Vuzo kutoka kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIS Nairobi na kumueleza matahali Kenya vijana wanapaswa kufanya nini ili kuchangia katika maendeleo.

Duration:00:03:26

Ask host to enable sharing for playback control

Mtoto aliyebakwa na kutiwa ujauzito DRC asema "siko tayari kuwa mama"

4/11/2025
Mtoto mmoja alibakwa katika kila nusu saa huko Mashariki mwa Jamhuri ya ya Kidemokrasia ya Congo, DRC wakati mapigano yaliposhika kasi mwanzoni mwa mwaka huu kati ya jeshi la serikali FARDC na waasi wa M23, katikati ya ufadhili finyu wa kifedha, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF. Anold Kayanda na maelezo zaidi.

Duration:00:01:58

Ask host to enable sharing for playback control

11 APRILI 2025

4/11/2025
Hii leo jaridani tunaangazia hali ya watoto nchini DR Congo, na masuala y awanawake nchini Tanzania. Makala inatupeleka nchini Kenya kuangazia harakati za vijana za kusongesha Ajenda2030, na mashinani tunasalia huko huko kumulika misaada kwa wakimbizi.Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF limeripoti kwamba huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kila nusu saa takribani mtoto mmoja anaripotiwa kubakwa huku ghasia zikiendelea katikati ya janga linalozidi kukua la ufadhili finyu wa kifedha.Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake UN WOMEN nchini Tanzania chini ya ufadhili kutoka Muungano wa Ulaya wanashirikiana na jeshi la polisi kuendesha mradi huko visiwani Zanzibar wa kukomesha unyanyasaji dhidi ya wanawake na wasichana na tayari manufaa ya mradi huo yameanza kuonekana.Makala leo inatupeleka Nairobi Kenya kwa Stella Vuzo kutoka kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIS Nairobi akizungumza na Winifred Njiru mwanafunzi wa chuo kikuu fani ya uhakiki au quantity surveyor aliyeshiriki majadiliano ya wiki iliyopita kuhusu malengo ya maendeleo endelevu yaliyoandaliwa na Club De Madri, anaeleza nini kama kijana anapaswa kufanya kuchangia ajenda hiyo ya maendeleo.Na katika mashinani Cindy McCain, Mkurugenzi Mtendaji wa WFP, akizungumza kutoka kituo cha shirika hilo kilichopo Mombasa, Kenya anaeleza juhudi wanazofanya kuwasaidia wakimbizi wa Sudan na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC."Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Duration:00:09:57

Ask host to enable sharing for playback control

Dawati la jinsia katika vituo vya polisi laleta mabadiliko chanya visiwani Zanzibar nchini Tanzania

4/11/2025
Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake UN WOMEN nchini Tanzania chini ya ufadhili kutoka Muungano wa Ulaya wanashirikiana na jeshi la polisi kuendesha mradi huko visiwani Zanzibar wa kukomesha unyanyasaji dhidi ya wanawake na wasichana na tayari manufaa ya mradi huo yameanza kuonekana.

Duration:00:01:29

Ask host to enable sharing for playback control

Jifunze Kiswahili: Maana za neno "FIFILIZA"

4/10/2025
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi kutoka Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana za neno "FIFILIZA"
Ask host to enable sharing for playback control

10 APRILI 2025

4/10/2025
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo Idhaa hii inazungumza na Mwenyekiti wa Tanzania Women Ecocomic Empowerment Network (TAWEN), ambaye pia ni mchumi mbobezi Bi. Janet Zebedayo Mbene. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na neno la wiki.Shukran Anold na leo tunaanzia huko Geneva Uswisi ambapo shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO limetoa muongozo wake wa kwanza duniani wa kutambua, kutoa matibabu kwa haraka na matibabu ya muda mrefu kwa ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo.Nchini Chad katika mpaka wake na Sudan ambako Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR Filippo Grandi ametembelea na kuzungumza na wakimbizi wa Sudan pamoja na kujionea hali zao wakati huu ambapo wamepunguza kutoa chakula, malazi , maji na dawa na kauli yake ikawa moja tu, “Ninatoa wito kwa wafadhili, tafadhali msipunguze msaada kwa wathirika wa vita vya Sudan.”.Taarifa ya pamoja ya mashirika ya kibinadamu inayotolewa kila baada ya wiki mbili imeeleza kuhusu hali katika Ukanda wa Gaza inasema kuwa watu wanazidi kuuwawa na kujeruhiwa. Kwa zaidi ya mwezi sasa hakuna misafara ya misaada inayoruhusiwa kuingia Gaza. Watu kulazimishwa kuhama kinguvu kunaendelea, makazi ya wakimbizi yamefikia pomoni, huduma za usafi na kujisafi nazo ni mbaya.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi kutoka Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana za neno "FIFILIZA"Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Duration:00:09:59

Ask host to enable sharing for playback control

UNICEF na wadau Kenya waelekea kufanikisha ndoto ya Sharlyne kuwa mwandishi wa habari

4/9/2025
Kutana na Shalyne Kaputa, mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 16 kutoka kaunti ya Turkana, Kaskazini-Magharibi mwa Kenya. Tofauti na shangazi yake, ambaye hakuweza kuendelea na elimu yake kutokana na kukosa karo, yeye anasoma elimu ya sekondari sasa ili aweze kutimiza ndoto yake ya kuwa mwandishi wa habari. Yote yanawezekana kutokana na mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF kwa msaada wa shirika la Norway la Maendeleo NORAD na wadau wengine. Je ni usaidizi gani wanapatiwa? Ungana na Assumpta Massoi.

Duration:00:04:24

Ask host to enable sharing for playback control

Lazima hatua madhubuti zichukuliwe kukomesha mzunguko wa watu kutoweka nchini Sudan - Radhouane Nouicer

4/9/2025
Wakati hofu ikiendelea kuhusu watu kutoweka kwa wingi nchini Sudan, Mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa aliyeteuliwa na Ofisi ya Haki za Binadamu OHCHR anayehusika na haki za binadamu nchini humo Radhouane Nouicer ametoa wito wa dharura kuhusu hali ya raia waliokwama katika vita kubwa nchini humo. Flora Nducha na taarifa zaidi.

Duration:00:03:22

Ask host to enable sharing for playback control

09 APRILI 2025

4/9/2025
Hii leo jaridani tunaangazia hali ya kibinadamu katika katika jimbo la Upper Nile nchini Sudan, na haki za binadamu na watu kutoweka kwa wingi nchini Sudan. Makala inatupeleka nchini Kenya na Mashinani tunakwenda Gaza, kulikoni?Nchini Sudan Kusini, familia zilizo kwenye hali duni katika eneo la kaskazini mashariki mwa nchi hiyo ziko katika hali tete sana huku mapigano yakizidi kuongezeka na njaa ikikaribia kufikia viwango vya juu kabisa, limeonya leo Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP).Wakati hofu ikiendelea kuhusu watu kutoweka kwa wingi nchini Sudan, Mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa aliyeteuliwa na Ofisi ya Haki za Binadamu OHCHR anayehusika na haki za binadamu nchini humo Radhouane Nouicer ametoa wito wa dharura kuhusu hali ya raia waliokwama katika vita kubwa nchini humo.Katika inatupeleka nchini Kenya kufuatilia simulizi ya Shalyne Kaputa, mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 16 kutoka kaunti ya Turkana ambaye tofauti na shangazi yake ambaye hakuweza kuendelea na elimu yake kutokana na kukosa karo, yeye anasoma elimu ya sekondari sasa ili aweze kutimiza ndoto yake ya kuwa mwandishi wa habari. Yote yanawezekana kutokana na mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF kwa msaada wa shirika la Norway la Maendeleo NORAD na wadau wengine.Na mashinani fursa ni yake Lama, mtoto mwenye umri wa miaka 10 kutoka Gaza eneo la Palestina linalokaliwa na Israeli ambaye anasimulia maumivu na juhudi za kila siku za kutafuta maji mapigano yakiwa ni mwaka mmoja na nusu sasa. Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) linatoa msaada mkubwa kwa familia na watoto wa Gaza kwa kusambaza maji salama.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Duration:00:12:09

Ask host to enable sharing for playback control

Ukosefu wa usalama wanyima chakula wahitaji Upper Nile nchini Sudan Kusini

4/9/2025
Nchini Sudan Kusini, familia zilizo kwenye hali duni katika eneo la kaskazini mashariki mwa nchi hiyo ziko katika hali tete sana huku mapigano yakizidi kuongezeka na njaa ikikaribia kufikia viwango vya juu kabisa, limeonya leo Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP). Anold Kayanda na maelezo zaidi.

Duration:00:01:46

Ask host to enable sharing for playback control

08 APRILI 2025

4/8/2025
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika shughuli za shirika lisilo la kiserikali la KINNAPA Development Programme la huko nchini Tanzania katika kutekeleza Malengo ya Maendeleo Endelevu likijikita zaidi katika usawa wa kijinsia. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani:Uganda, ambayo tayari ni mwenyeji wa wakimbizi wengi zaidi barani Afrika, inakabiliwa na shinikizo kubwa baada ya wakimbizi zaidi ya 41,000 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC kuingia nchini humo tangu Januari mwaka huu, wakikimbia machafuko mapya mashariki mwa nchi yao limesema leo Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR. UNHCR imesema watu walioko katika mazingira hatarishi wanatambuliwa kwa msaada maalum, huku familia zilizotengana zikisaidiwa kuunganishwa tena.Siku kumi baada ya matetemeko ya ardhi ya kutisha yaliyoitikisa Myanmar tarehe 28 Machi, idadi ya vifo inaendelea kuongezeka. Titon Mitra, Mwakilishi wa Kikanda wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo UNDP nchini humo, akiripoti leo akiwa katika jiji liloharibiwa sana la Mandalay, kwa njia ya video ameripoti kwa waandishi wa habari jijini Geneva, Uswisi akisema, “idadi ya vifo ya hivi karibuni imepita watu 3,500 na “inaweza kuendelea kuongezeka.”Kenya, Uganda na Rwanda zitanufaika na mpango wa mlo shuleni baada ya leo Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) kutangaza kuwa linaendeleza ushirikiano wake na Taasisi ya Novo Nordisk, kupitia ushirikiano wa kihistoria kati ya sekta binafsi na ya umma unaojumuisha Wizara ya Mambo ya Nje ya Denmark na Taasisi ya Grundfos, ili kupanua mpango wa mlo shuleni kutokana na chakula kinachozalishwa ndani ya nchi husika. Ushirikiano huu utajenga mfumo wa msaada unaohakikisha uendelevu wa muda mrefu wa mpango huu.Na mashinani mashinani jana tarehe 7 Aprili hapa Umoja wa Mataifa kumefanyika kumbukizi ya miaka 31 ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda ambapo mmoja wa wazungumzaji alikuwa Germaine Tuyisenge Müller, manusura wa mauaji hayo na wakati huo alikuwa na umri wa miaka 9 wakiishi mji mkuu Kigali.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Duration:00:11:50

Ask host to enable sharing for playback control

DaySpring Foundation nchini Tanzania yatekeleza kivitendo dhana ya UN ya michezo kwa maendeleo

4/7/2025
Siku ya kimataifa ya Michezo kwa ajili ya Maendeleo na Amani imeadhimishwa tarehe 6 mwezi huu wa Aprili maudhui yakiwa Ujumuishaji wa kijamii, hususan makundi ya pembezoni. Umoja wa Mataifa kupitia wavuti wake unasema kuwa siku hii inatambuliwa kutokana na nafasi ya michezo katika kuleta mabadiliko chanya, kuondoa vikwazo na kuvuka mipaka. Na usuli wa maudhui ya mwaka huu ni kwamba fikra potofu kwenye jamii zimesababisha baadhi ya watu kutokana na jinsia yao, umri, au rangi wanashindwa kushiriki kwenye michezo ambayo kwa njia moja au nyingine hutokomeza umaskini kwa kuwezesha washiriki kujipatia kipato. Nchini Tanzania shirika la kiraia la DaySpring Foundation limetambua nafasi ya michezo na limeanza kuchukua hatua. Assumpta Massoi wa Idhaa hii amezungumza na Muasisi na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, Rosemary Mwaipopo ambaye anaanza kwa kuelezea ni kwa nini waliamua kujikita katika kusaka vipaji.

Duration:00:04:04

Ask host to enable sharing for playback control

Kwibuka2025: Katibu Mkuu UN ahimiza mshikamano wa kimataifa dhidi ya chuki

4/7/2025
Dunia inapokumbuka miaka 31 tangu mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi nchini Rwanda mwaka 1994, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametuma ujumbe mzito wa maombolezo na onyo, akitaka mshikamano wa kimataifa kupambana na ongezeko la chuki, mgawanyiko, na misimamo mikali kupitia mifumo ya kidijitali. Anold Kayanda na maelezo zaidi.

Duration:00:02:12

Ask host to enable sharing for playback control

07 APRILI 2025

4/7/2025
Hii leo jaridani tunaangazia makumbusho ya mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi nchini Rwanda mwaka 1994, na Siku ya Afya Duniani. Makala inamulika nafasi ya michezo katika kusongesha amani na maendeleo, na mashinani tunakwenda nchini Kenya, kulikoni?Dunia inapokumbuka miaka 31 tangu mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi nchini Rwanda mwaka 1994, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametuma ujumbe mzito wa maombolezo na onyo, akitaka mshikamano wa kimataifa kupambana na ongezeko la chuki, mgawanyiko, na misimamo mikali kupitia mifumo ya kidijitali.Leo ni Siku ya Afya Duniani ambayo mwaka huu inangazia suala muhimu kwa afya ya dunia, changamoto maalum wanazokumbana nazo wanawake na wasichana lakini pia vifo vya watoto wachanga, na ili kuhakikisha changamoto hizo zinashughulikiwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani WHO limezindua kampeni ya mwaka mzima ya “Mwanzo wenye afya ni mustakbali wenye matumaini”..Makala inamulika nafasi ya michezo katika kusongesha amani na maendeleo, ambapo Assumpta Massoi amezungumza na Rosemary Mwaipopo, Muasisi na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la kiraia la DaySpring Foundation nchini Tanzania. Yeye alikuwa ni miongoni mwa washiriki wa Mkutano wa 69 wa Hali ya Wanawake duniani, CSW69 uliofanyika hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa mwezi uliopita wa Machi.Na mashinanileo ikiwa leo ni siku ya afya duniani, kupitia mahojiano yaliyofanikishwa na washirika wetu Radio Domus, fursa ni yake Padri Thaddeus Mukaya wa kanisa la katoliki la Parokia ya Embulbul ambalo pamoja na wadau wengine waliandaa huduma za bure za matibabu kwa wenyeji wa eneo hilo ili kusaidia jamii ambazo haziwezi kujimudu kimaisha.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Duration:00:11:47

Ask host to enable sharing for playback control

Hatua za haraka zinahitajika sasa kuzuia vifo na kulinda afya ya wanawake na wasichana: UN

4/7/2025
Leo ni Siku ya Afya Duniani ambayo mwaka huu inangazia suala muhimu kwa afya ya dunia, changamoto maalum wanazokumbana nazo wanawake na wasichana lakini pia vifo vya watoto wachanga, na ili kuhakikisha changamoto hizo zinashughulikiwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani WHO limezindua kampeni ya mwaka mzima ya “Mwanzo wenye afya ni mustakbali wenye matumaini”. Flora Nducha anafafanua zaidi.

Duration:00:02:40

Ask host to enable sharing for playback control

Uongozi bora na matumizi bora ya rasilimali vitaikomboa Afrika kimaendeleo: Vijana Kenya

4/4/2025
Majadiliano ya siku mbili yanayofanyika kila mwaka ya será kuhusu maendeleo endelevu. Majadiliano hayo yanayokunja jamvi leo jijini Nairobi Kenya yameandaliwa na Club De Madrid na mwaka huu yakijikita na ufadhili wa maendeleo na kuwaleta pamoja wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wastaafu w anchi na serikali, wadau wa maendeleo na vijana. Stella Vuzo kutoka kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIS Nairobi amepata fursa ya kuzungumza na baadhi ya vijana wanaoshiriki mkutano huo wa club de Madrid je wanasemaje? Ungana nao katika makala hii

Duration:00:03:22

Ask host to enable sharing for playback control

Umoja wa Mataifa kuendelea kuisaidia Somalia kuonda mabomu ya kutegwa ardhini

4/4/2025
Ikiwa leo ni Siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu mabomu ya kutegwa ardhini na Msaada wa Hatua Dhidi ya Mabomu hayo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akisisitiza mataifa duniani kote kuheshimu mikataba ya kimataifa dhidi ya vilipuzi na silaha nyingine, Umoja wa Mataifa leo umethibitisha tena dhamira yake ya kusaidia Somalia katika mapambano dhidi ya hatari za vilipuzi kwa ajili ya mustakabali salama kwa Wasomali wote. Anold Kayanda na taarifa zaidi.

Duration:00:01:52

Ask host to enable sharing for playback control

04 APRILI 2025

4/4/2025
Hii leo jaridani tunaangazia Siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu mabomu ya kutegwa ardhini. Makala inamulika harakati za kusongesha malengo ya maendeleo endelevu ikitupeleka nchini Kenya na mashinani tunasalia huko huko nchini Kenya, kulikoni?Ikiwa leo ni Siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu mabomu ya kutegwa ardhini na Msaada wa Hatua Dhidi ya Mabomu hayo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akisisitiza nchi kuheshimu mikataba ya kimataifa dhidi ya vilipuzi na silaha nyingine, Umoja wa Mataifa leo umethibitisha tena dhamira yake ya kusaidia Somalia katika mapambano dhidi ya hatari za vilipuzi kwa ajili ya mustakabali salama kwa Wasomali wote.Mwaka huu wa 2025, Siku ya Kimataifa ya Uhamasishaji Kuhusu Mabomu ya Ardhi na Usaidizi kwa Hatua Dhidi ya Mabomu inaadhimishwa chini ya kaulimbiu “Mustakabali Salama Unaanzia Hapa.” Umoja wa Mataifa inasisitiza umuhimu wa kufadhili miradi midogo yenye athari za haraka kusaidia watu wenye ulemavu wa viungo waliathirika katika mizozo. Juhudi hizi zinaimarisha ulinzi wa raia na kupanua teknolojia na uvumbuzi katika nchi zinazoendelea.Makala ambayo inamulika majadiliano ya siku mbili yanayofanyika kila mwaka ya será kuhusu maendeleo endelevu. Majadiliano hayo yanayokunja jamvi leo jijini Nairobi Kenya yameandaliwa na Club De Madrid na mwaka huu yamejikita na ufadhili wa maendeleo, Stella Vuzo kutoka kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIS Nairobi amepata fursa ya kuzungumza na baadhi ya vijana wanaoshiriki mkutano huo wa club de Madrid.Na mashinani leo utamsikia mhadhiri kutoka chuo kikuu cha Bayero jimboni Kano nchini Nigeria anayeshiriki mkutano wa majadiliano ya ufadhili wa maendeleo endelevu unaofanyika Nairobi Kenya.Mwenyeji wako ni Assumpta, karibu!

Duration:00:09:59

Ask host to enable sharing for playback control

Uteguaji mabomu ya ardhini ni suala la amani na kiutu - UNMAS

4/4/2025
Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu mabomu ya kutegwa ardhini, kauli mbiu ikiwa Mustakabali salama unaanzia hapa, Umoja wa Mataifa unasisitiza umuhimu wa kufadhili miradi midogo yenye matokeo chanya na ya haraka ili kusaidia sio tu watu wanaopata ulemavu wa viungo kutokana na madhara ya mabomu hayo bali pia kuwezesha watu kurejea kwenye maisha yao ya kawaida Sharon Jebichii anamulika Lebanon na Libya.

Duration:00:02:00

Ask host to enable sharing for playback control

Jifunze Kiswahili: Maana ya neno "MHARUMA.”

4/3/2025
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "MHARUMA.”