
Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
United Nations
Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Location:
New Rochelle, NY
Genres:
News & Politics Podcasts
Networks:
United Nations
Description:
Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Twitter:
@HabarizaUN
Language:
Swahili
Contact:
9178215291
Episodes
Uhaba wa fedha watishia ukarimu wa Zambia kwa wakimbizi - UNHCR
4/16/2025
Zambia inaendelea kuwahifadhi zaidi ya wakimbizi 106,000, wengi wao wakiwa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Burundi, pamoja na wakimbizi wa zamani kutoka Rwanda na Angola, kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR, ambalo limesema kwa kuzingatia sera yake jumuishi, nchi hiyo inakuza mshikamano na wakimbizi na kuwawezesha kujitegemea kupitia makazi maalum na ushirikiano na jamii za wenyeji. Flora Nducha na taarifa zaidi Shirika hilo la wakimbizi limesema katika makazi kama Mayukwayukwa na Maheba ambayo ni moja ya kambi kubwa zaidi ya wakimbizi nchini Zambia familia za wakimbizi zilizolazimika kukimbia makwao zinajumuishwa ili ziweze kujikimu na kuishi kwa utangamano na wenyeji wanaowahifadhi. Moulid Hujale, ni afisa habari msaidizi wa UNHCR anasema “Selikali ya Zambia inajumuisha wakimbizi katika huduma za kitaifa kama vile elimu na hata programu za msaada wa kilimo ili kuongeza uzalishaji” Amebainisha kuwa kwa kufanya hivyo Zambia imeonesha mshikamano wa dhati kwa jamii hizo za wakimbizi kwa kuhakikisha kuwa wanapata fursa ya kujenga upya maisha yao, kujikwamua kiuchumi na kuishi kwa heshima.Hata hivyo, UNHCR inasema nchi hiyo ya Kusini mwa Afrika pamoja na ukarimu wake bado inakumbwa na athari za ukame mkali uliotishia uhakika wa chakula na kuyumbisha uchumi na katika hatua za kukabiliana na hali hiyo, Moulid ansema “UNHCR inashirikiana na serikali ya Zambia kuunganisha makazi ya wakimbizi kwenye gridi ya taifa ya umeme. Tunajua muundo huu wa ujumuishwaji na maisha endelevu vinagharimu fedha, Lakini hiki ndicho hasa wakimbizi wanachokihitaji, hivyo tunahitaji msaada wako ili kufanikisha hili”. Licha ya mafanikio yaliyopatikana hadi sasa Zambia katika kuwakirimu wakimbizi, UNHCR imeonya kuwa uhaba wa fedha inaokabiliwa nao unatishia kuathiri mafanikio hayo na hasa utoaji wa huduma muhimu kwa familia hizo zilizolazimika kufungasha virago na kusaka usalama Zambia. Sasa limetoa ombi la msaada wa haraka wa kimataifa ili kuendelea kufanikisha huduma za kuokoa maisha zinazohitajika sana na wakimbizi hao.
Duration:00:02:05
16 APRILI 2025
4/16/2025
Hii leo jaridani Assumpta Massoi anamulika masuala ya afya hususan harakati za kukabiliana na majanga yajayo ya afya; wakimbizi huko Zambia ambako sera jumuishi zimewajengea uwezo; Jukwaa la vijana na mchango wa sanaa kwenye usawa na utengamano. Baada ya zaidi ya miaka mitatu ya mazungumzo ya kina, hatimaye leo huko mjini Geneva, Uswisi, nchi wanachama wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) zimekamilisha rasimu ya makubaliano ambayo itawasilishwa katika Mkutano wa Afya Duniani mwezi ujao wa Mei. Pendekezo hili linakusudia kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika kuzuia, kujiandaa na kukabiliana na vitisho vya majanga ya kiafya yajayo. Anold Kayanda amefuatilia anatujulisha zaidi.Zambia inaendelea kuwahifadhi zaidi ya wakimbizi 106,000, wengi wao wakiwa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Burundi, pamoja na wakimbizi wa zamani kutoka Rwanda na Angola. Limesema shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR, likiongeza kwamba kwa kuzingatia sera jumuishi ya Zambia, taifa hilo linakuza mshikamano na wakimbizi na kuwawezesha kujitegemea kupitia makazi maalum na ushirikiano na jamii za wenyeji. Flora Nducha na taarifa zaidi.Jukwaa la Vijana la Baraza la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Kiuchumi na Kijamii (ECOSOC) limeanza jana hapa katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa na litamalizika kesho tarehe 17 Aprili. Vijana kutoka nchi mbalimbali wamehudhuria jukwaa hilo akiwemo Kapwani Kavenuke kutoka nchini Tanzania ambaye amehojiwa na Leah Mushi wa Idhaa hii. Kapwani anaanza kwa kueleza umuhimu wa mikutano hii.Gislain Kalwira, Muandaaji wa tamasha la Musika na Kipaji nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC linalofanyika kila mwaka kuleta pamoja wasanii wa kike na wa kiume wa fani mbalimbali, kwa kutambua kuwa jana dunia imeadhimisha siku ya sanaa duniani. Kalwira kupitia video iliyochapishwa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini DRC, MONUSCO, anafafanua mantiki ya tamasha hilo na kujenga usawa kijinsia.
Duration:00:09:57
Wanachama wa WHO wachukua hatua za kujenga uwezo dhidi ya majanga yajayo ya afya
4/16/2025
Baada ya zaidi ya miaka mitatu ya mazungumzo ya kina, hatimaye leo Geneva, Uswisi, Nchi Wanachama wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) zimekamilisha rasimu ya makubaliano ambayo itawasilishwa katika Mkutano wa Afya Duniani mwezi Mei mwaka huu wa 2025. Pendekezo hili linakusudia kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika kuzuia, kujiandaa na kukabiliana na vitisho vya majanga ya kiafya yajayo. Anold Kayanda amefuatilia anatujulisha zaidi. "Leo mataifa ya dunia yameandika historia mjini Geneva," amesema Dkt. Tedros Ghebreyesus, Mkurugenzi Mkuu wa WHO na kuongeza kwamba, "kwa kufikia makubaliano kuhusu Mkataba wa Majanga ya kiafya, siyo tu wameweka msingi wa makubaliano ya kizazi hiki yanayolenga kuifanya dunia kuwa salama zaidi, bali pia wameonesha kuwa ushirikiano wa kimataifa bado uko hai, na kwamba hata katika dunia iliyogawanyika, mataifa bado yanaweza kushirikiana kutafuta mwafaka na mwitikio wa pamoja dhidi ya vitisho vya pamoja.” Mwezi Desemba mwaka 2021, wakati janga la COVID-19 likiwa limepamba moto, Nchi Wanachama wa WHO ziliunda Mamlaka ya Majadiliano ya Kiserikali ili kuandaa na kujadiliana kuhusu mkataba, makubaliano au nyenzo nyingine ya kimataifa, chini ya Katiba ya WHO, kwa ajili ya kuimarisha uzuiaji, maandalizi na hatua dhidi ya majanga ya kiafya. Mapendekezo katika rasimu iliyotayarishwa ni pamoja na: kuchukua hatua madhubuti za kuzuia majanga ya kiafya kwa kutumia mbinu ya Afya Moja; kujenga uwezo wa utafiti na maendeleo katika maeneo mbalimbali duniani; kuwezesha uhamishaji wa teknolojia na maarifa, ujuzi na utaalamu unaohusiana na uzalishaji wa bidhaa za afya zinazohusiana na majanga ya kiafya; kuchukua hatua madhubuti za kuimarisha maandalizi, utayari na uimara wa mifumo ya afya; na kuanzisha mtandao wa kimataifa wa mnyororo wa usambazaji na vifaa. Pendekezo hilo linathibitisha mamlaka ya nchi kushughulikia masuala ya afya ya umma ndani ya mipaka yao bila kuingiliwa.
Duration:00:01:50
Jamii inapaswa kusikiliza na kujifunza kutoka kwa vijana
4/16/2025
Jukwaa la Vijana la Baraza la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Kiuchumi na Kijamii (ECOSOC) linafanyika katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani ambapo limeanza tarehe 15 Aprili na linatarajiwa kukamilika tarehe 17 Aprili 2025. Vijana kutoka nchi mbalimbali pamoja na wadau wengine wa masuala ya maendeleo na Uchumi wanakuja pamoja kujadili changamoto mbalimbali na namna bora ya kupatia ufumbuzi katika kuubadilisha ulimwengu kuwa mahali penye usawa zaidi na endelevu chini ya mwongozo wa Ajenda ya mwaka 2030 na Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs). Miongoni mwa wanaohudhuria jukwaa hilo ni Kapwani Kavenuke kutoka nchini Tanzania ambaye amefanyiwa mahojiano na Leah Mushi na hapa anaanza kwa kueleza umuhimu wa mikutano huo.
Duration:00:03:42
15 Aprili 2025
4/15/2025
Karibu kusikiliza jarida la Umoja wa Mataifa ambapo hii leo tunamulika Kongamano la Kimataifa la Kiswahili linalofanyika mjini Kampala Uganda likiwaleta pamoja wadau kutoka kila kona ya Afrika na kwingineko kujadili mikakati ya kukuza lugha hiyo adhimu ya Kiswahili. Utasikiliza muhtasari wa habari ukiangazia miaka miwili tangu kuanza kwa vita vya sasa vya Sudan, UNHCR, yatoa wito kwamba mwitiko mkubwa wa kibinadamu ulioratibiwa vema ni muhimu ili kuzuia mateso zaidi na vifo kwa wananchi wa DRC, na Jukwaa la Vijana la Baraza la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Kiuchumi na Kijamii (ECOSOC) limeanza leo tarehe 15 hadi tarehe 17 katika Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani.
Duration:00:09:59
Vita Sudan yamsababishia Walaa tatizo la afya ya akili
4/14/2025
Tarehe 15 mwezi April imwaka 2023 wananchi wa Sudan hususan mji mkuu Khartoum waliamshwa na mapigano kati ya jeshi la serikali SAF na wanamgambo wa kikosi cha msaada wa haraka RSF. Hadi leo hii mapigano hayo yanazidi kushika kasi na raia wanafurushwa makwao. Miongoni mwao ni watoto ambao zahma wanayokutana nayo sio tu kufurushwa bali pia changamoto ya afya ya akili. Tayari shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limeona shida hiyo na limeanza kuchukua hatua kama anavyosimulia Assumpta Massoi kwenye makala hii.
Duration:00:03:46
Chonde chonde tusiipe kisogo Sudan: Nkweta-Salami
4/14/2025
Sudan Clementine Nkweta-Salami, Mwakilishi Mkazi na Mratibu wa Masuala ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan akizungumza na UN News amesema hali si hali kama anavyofafanua Flora Nducha.(TAARIFA YA FLORA NDUCHA)Bi Nkweta-Salami amesema ufurushwaji wa watu unaendelea, mahitaji ni makubwa sana, tayari baa la njaa limeshabainika katika baadhi ya maeneo ya nchi, na wanakimbizana na muda kuzuia baa hilo lisienee zaidi.(SAUTI CLEMENTINE 1-SABRINA)"Hali ya kibinadamu ni ya kutisha, bado tunahaha. Hatuna uwezo wa kufikia maeneo yote yenye machafuko. Tunajitahidi kuhakikisha kwamba rasilimali tulizo nazo zinaweza kufikishwa haraka iwezekanavyo kwa kutumia njia zote tulizo nazo. Watu milioni 12 wametawanywa. Kwa ujumla, bado tunahitaji juhudi kubwa, ado tunahitaji msaada kutoka kwa jumuiya ya kimataifa kwa upande wa rasilimali, na bado tunahitaji msaada zaidi wa kuruhusu utoaji wa misaada kutoka kwa makundi yote yenye silaha yanayohusika katika mzozo huu.”Licha ya kukosena suhuhu ya kisasa hadi sasa amesema wataendelea kusaidia wenye uhitaji(CLEMENTINE 2-SABRINA)“Msaada wa kibinadamu unapaswa kuendelea hata kama hakuna suluhisho la kisiasa kwa mzozo huu, na hata kama hakuna makubaliano ya kusitisha mapigano. Tunaendelea kushirikiana na jumuiya ya kimataifa na nchi wanachama zinazoshiriki kwenye majadiliano na mazungumzo ya kisiasa kujaribu kutumia majadiliano hayo kuwezesha kazi zetu kupitia usitishaji wa muda wa mapigano na kujaribu kuwashawishi makundi yenye silaha kukubaliana na njia ambazo tunaweza kutumia bila kuhatarisha maisha kwa kushambuliwa, kulipuliwa au kupigwa makombora”.Na rai yake ni kwamba(CLEMENTINE 3-SABRINA)Watu wako katika hali ya zahma kubwa, msaada unahitajika na tunatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kutowasahau watu wa Sudan wanaume, wanawake na watoto wanaojikuta katika hali hii ngumu sana kwa sasa.TAGS: Sudan, Vita, amani na usalama, msaada wa kibinadamu
Duration:00:02:07
Tume huru ya UN ya kusaka ukweli kuhusu Sudan imelaani vikali mauaji ya watu zaidi ya 100
4/14/2025
Vita ya sasa ya Sudan ikielekea kuingia mwaka wa tatu, Tume Huru ya Umoja wa Mataifa ya kusaka ukweli kuhusu Sudan imelaani vikali mauaji ya watu zaidi ya 100 yaliyotokea wikiendi hii katika kambi za wakimbizi wa ndani Darfur, ikionya kwamba hali inaweza kuwa mbaya zaidi. Anold Kayanda na taarifa zaidi.(Taarifa ya Anold Kayanda)Shukrani LeahTangu kuanza kwa vita kati ya Jeshi la Sudan (SAF) na kikosi cha waasi cha RSF mnamo tarehe 15 Aprili mwaka 2023, maelfu ya watu wamepoteza maisha, huku mamilioni wakikumbwa na njaa, ubakaji, na ufurushwaji. Kambi kama ya Zamzam, yenye wakazi zaidi ya laki saba – nusu yao wakiwa watoto – zinaripotiwa kuzingirwa, wakazi wake wakikosa chakula, dawa, na maji, imeeleza Tume Huru ya Umoja wa Mataifa ya kusaka ukweli kuhusu Sudan.Mwenyekiti wa tume hiyo, Mohamed Chande Othman, ananukuliwa akisema, “Dunia imeshuhudia miaka miwili ya mzozo usio na huruma ambao umewanasa mamilioni ya raia katika mazingira ya kutisha, wakiwekwa katika hali ya ukatili bila matumaini ya mwisho.”Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, Catherine Russell kuhusu tukio hili la hivi karibuni ni kwamba watoto takriban 23 na wahudumu 9 wa misaada wameripotiwa kuuawa katika mfululizo wa mashambulizi katika eneo la Darfur Kaskazini, katika kipindi cha siku tatu zilizopita.Jana Jumapili, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amesisitiza kuwa mashambulizi yanayolenga raia ni marufuku kabisa chini ya sheria ya kimataifa ya kibinadamu. Wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu na wafanyakazi wa afya wanapaswa kuheshimiwa na kulindwa,anasema.Kesho Jumanne huko London Uingereza, mataifa takriban 20 yanatarajiwa kujadili hali ya kibinadamu nchini Sudan. Umoja wa Mataifa unatoa wito wa hatua za haraka kulinda raia, kusitisha uungwaji mkono kwa pande zinazopigana, na kuhakikisha haki na uwajibikaji kwa uhalifu wa kivita.
Duration:00:02:02
14 APRILI 2025
4/14/2025
Vita Sudan vikiingia mwaka wa tatu, Tume Huru ya UN yalaani mauaji ya Darfur, Sudan.Chonde chonde tusiipe kisogo Sudan: Nkweta-Salami.Makala inatupeleka jimboni Kassala mashariki mwa Sudan.Na mashinani tutasalia Sudan ambako vita vimechochea ongezeko la utapiamlo kwa watoto.
Duration:00:10:48
Vijana tuna jukumu muhimu katika maendeleo ya jamii zetu tuchangamkie fursa: Winfred Njiru
4/11/2025
Umoja wa Mataifa unaendelea kuchagiza vijana kujitokeza na kushiriki katika kusongesha ajenda ya maendeleo endelevu katika jamii zao na ndio maana wiki iliyopita majadiliano ya viongozi wastaafu kuhusu maendeleo endelevu ya Club De Madrid yaliyofanyika Nairobi Kenya yalitoa fursa kwa vijana kupaza sauti zao kuhusu jinsi wataavyochangia kufanikisha malengo hayo. Winfred Njiru mwanafunzi wa chuo kikuu fani ya uhakiki au quantity surveyor alizungumza na Stella Vuzo kutoka kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIS Nairobi na kumueleza matahali Kenya vijana wanapaswa kufanya nini ili kuchangia katika maendeleo.
Duration:00:03:26
Mtoto aliyebakwa na kutiwa ujauzito DRC asema "siko tayari kuwa mama"
4/11/2025
Mtoto mmoja alibakwa katika kila nusu saa huko Mashariki mwa Jamhuri ya ya Kidemokrasia ya Congo, DRC wakati mapigano yaliposhika kasi mwanzoni mwa mwaka huu kati ya jeshi la serikali FARDC na waasi wa M23, katikati ya ufadhili finyu wa kifedha, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF. Anold Kayanda na maelezo zaidi.
Duration:00:01:58
11 APRILI 2025
4/11/2025
Hii leo jaridani tunaangazia hali ya watoto nchini DR Congo, na masuala y awanawake nchini Tanzania. Makala inatupeleka nchini Kenya kuangazia harakati za vijana za kusongesha Ajenda2030, na mashinani tunasalia huko huko kumulika misaada kwa wakimbizi.Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF limeripoti kwamba huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kila nusu saa takribani mtoto mmoja anaripotiwa kubakwa huku ghasia zikiendelea katikati ya janga linalozidi kukua la ufadhili finyu wa kifedha.Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake UN WOMEN nchini Tanzania chini ya ufadhili kutoka Muungano wa Ulaya wanashirikiana na jeshi la polisi kuendesha mradi huko visiwani Zanzibar wa kukomesha unyanyasaji dhidi ya wanawake na wasichana na tayari manufaa ya mradi huo yameanza kuonekana.Makala leo inatupeleka Nairobi Kenya kwa Stella Vuzo kutoka kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIS Nairobi akizungumza na Winifred Njiru mwanafunzi wa chuo kikuu fani ya uhakiki au quantity surveyor aliyeshiriki majadiliano ya wiki iliyopita kuhusu malengo ya maendeleo endelevu yaliyoandaliwa na Club De Madri, anaeleza nini kama kijana anapaswa kufanya kuchangia ajenda hiyo ya maendeleo.Na katika mashinani Cindy McCain, Mkurugenzi Mtendaji wa WFP, akizungumza kutoka kituo cha shirika hilo kilichopo Mombasa, Kenya anaeleza juhudi wanazofanya kuwasaidia wakimbizi wa Sudan na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC."Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Duration:00:09:57
Dawati la jinsia katika vituo vya polisi laleta mabadiliko chanya visiwani Zanzibar nchini Tanzania
4/11/2025
Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake UN WOMEN nchini Tanzania chini ya ufadhili kutoka Muungano wa Ulaya wanashirikiana na jeshi la polisi kuendesha mradi huko visiwani Zanzibar wa kukomesha unyanyasaji dhidi ya wanawake na wasichana na tayari manufaa ya mradi huo yameanza kuonekana.
Duration:00:01:29
Jifunze Kiswahili: Maana za neno "FIFILIZA"
4/10/2025
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi kutoka Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana za neno "FIFILIZA"
10 APRILI 2025
4/10/2025
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo Idhaa hii inazungumza na Mwenyekiti wa Tanzania Women Ecocomic Empowerment Network (TAWEN), ambaye pia ni mchumi mbobezi Bi. Janet Zebedayo Mbene. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na neno la wiki.Shukran Anold na leo tunaanzia huko Geneva Uswisi ambapo shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO limetoa muongozo wake wa kwanza duniani wa kutambua, kutoa matibabu kwa haraka na matibabu ya muda mrefu kwa ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo.Nchini Chad katika mpaka wake na Sudan ambako Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR Filippo Grandi ametembelea na kuzungumza na wakimbizi wa Sudan pamoja na kujionea hali zao wakati huu ambapo wamepunguza kutoa chakula, malazi , maji na dawa na kauli yake ikawa moja tu, “Ninatoa wito kwa wafadhili, tafadhali msipunguze msaada kwa wathirika wa vita vya Sudan.”.Taarifa ya pamoja ya mashirika ya kibinadamu inayotolewa kila baada ya wiki mbili imeeleza kuhusu hali katika Ukanda wa Gaza inasema kuwa watu wanazidi kuuwawa na kujeruhiwa. Kwa zaidi ya mwezi sasa hakuna misafara ya misaada inayoruhusiwa kuingia Gaza. Watu kulazimishwa kuhama kinguvu kunaendelea, makazi ya wakimbizi yamefikia pomoni, huduma za usafi na kujisafi nazo ni mbaya.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi kutoka Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana za neno "FIFILIZA"Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Duration:00:09:59
UNICEF na wadau Kenya waelekea kufanikisha ndoto ya Sharlyne kuwa mwandishi wa habari
4/9/2025
Kutana na Shalyne Kaputa, mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 16 kutoka kaunti ya Turkana, Kaskazini-Magharibi mwa Kenya. Tofauti na shangazi yake, ambaye hakuweza kuendelea na elimu yake kutokana na kukosa karo, yeye anasoma elimu ya sekondari sasa ili aweze kutimiza ndoto yake ya kuwa mwandishi wa habari. Yote yanawezekana kutokana na mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF kwa msaada wa shirika la Norway la Maendeleo NORAD na wadau wengine. Je ni usaidizi gani wanapatiwa? Ungana na Assumpta Massoi.
Duration:00:04:24
Lazima hatua madhubuti zichukuliwe kukomesha mzunguko wa watu kutoweka nchini Sudan - Radhouane Nouicer
4/9/2025
Wakati hofu ikiendelea kuhusu watu kutoweka kwa wingi nchini Sudan, Mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa aliyeteuliwa na Ofisi ya Haki za Binadamu OHCHR anayehusika na haki za binadamu nchini humo Radhouane Nouicer ametoa wito wa dharura kuhusu hali ya raia waliokwama katika vita kubwa nchini humo. Flora Nducha na taarifa zaidi.
Duration:00:03:22
09 APRILI 2025
4/9/2025
Hii leo jaridani tunaangazia hali ya kibinadamu katika katika jimbo la Upper Nile nchini Sudan, na haki za binadamu na watu kutoweka kwa wingi nchini Sudan. Makala inatupeleka nchini Kenya na Mashinani tunakwenda Gaza, kulikoni?Nchini Sudan Kusini, familia zilizo kwenye hali duni katika eneo la kaskazini mashariki mwa nchi hiyo ziko katika hali tete sana huku mapigano yakizidi kuongezeka na njaa ikikaribia kufikia viwango vya juu kabisa, limeonya leo Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP).Wakati hofu ikiendelea kuhusu watu kutoweka kwa wingi nchini Sudan, Mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa aliyeteuliwa na Ofisi ya Haki za Binadamu OHCHR anayehusika na haki za binadamu nchini humo Radhouane Nouicer ametoa wito wa dharura kuhusu hali ya raia waliokwama katika vita kubwa nchini humo.Katika inatupeleka nchini Kenya kufuatilia simulizi ya Shalyne Kaputa, mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 16 kutoka kaunti ya Turkana ambaye tofauti na shangazi yake ambaye hakuweza kuendelea na elimu yake kutokana na kukosa karo, yeye anasoma elimu ya sekondari sasa ili aweze kutimiza ndoto yake ya kuwa mwandishi wa habari. Yote yanawezekana kutokana na mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF kwa msaada wa shirika la Norway la Maendeleo NORAD na wadau wengine.Na mashinani fursa ni yake Lama, mtoto mwenye umri wa miaka 10 kutoka Gaza eneo la Palestina linalokaliwa na Israeli ambaye anasimulia maumivu na juhudi za kila siku za kutafuta maji mapigano yakiwa ni mwaka mmoja na nusu sasa. Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) linatoa msaada mkubwa kwa familia na watoto wa Gaza kwa kusambaza maji salama.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Duration:00:12:09
Ukosefu wa usalama wanyima chakula wahitaji Upper Nile nchini Sudan Kusini
4/9/2025
Nchini Sudan Kusini, familia zilizo kwenye hali duni katika eneo la kaskazini mashariki mwa nchi hiyo ziko katika hali tete sana huku mapigano yakizidi kuongezeka na njaa ikikaribia kufikia viwango vya juu kabisa, limeonya leo Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP). Anold Kayanda na maelezo zaidi.
Duration:00:01:46
08 APRILI 2025
4/8/2025
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika shughuli za shirika lisilo la kiserikali la KINNAPA Development Programme la huko nchini Tanzania katika kutekeleza Malengo ya Maendeleo Endelevu likijikita zaidi katika usawa wa kijinsia. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani:Uganda, ambayo tayari ni mwenyeji wa wakimbizi wengi zaidi barani Afrika, inakabiliwa na shinikizo kubwa baada ya wakimbizi zaidi ya 41,000 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC kuingia nchini humo tangu Januari mwaka huu, wakikimbia machafuko mapya mashariki mwa nchi yao limesema leo Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR. UNHCR imesema watu walioko katika mazingira hatarishi wanatambuliwa kwa msaada maalum, huku familia zilizotengana zikisaidiwa kuunganishwa tena.Siku kumi baada ya matetemeko ya ardhi ya kutisha yaliyoitikisa Myanmar tarehe 28 Machi, idadi ya vifo inaendelea kuongezeka. Titon Mitra, Mwakilishi wa Kikanda wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo UNDP nchini humo, akiripoti leo akiwa katika jiji liloharibiwa sana la Mandalay, kwa njia ya video ameripoti kwa waandishi wa habari jijini Geneva, Uswisi akisema, “idadi ya vifo ya hivi karibuni imepita watu 3,500 na “inaweza kuendelea kuongezeka.”Kenya, Uganda na Rwanda zitanufaika na mpango wa mlo shuleni baada ya leo Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) kutangaza kuwa linaendeleza ushirikiano wake na Taasisi ya Novo Nordisk, kupitia ushirikiano wa kihistoria kati ya sekta binafsi na ya umma unaojumuisha Wizara ya Mambo ya Nje ya Denmark na Taasisi ya Grundfos, ili kupanua mpango wa mlo shuleni kutokana na chakula kinachozalishwa ndani ya nchi husika. Ushirikiano huu utajenga mfumo wa msaada unaohakikisha uendelevu wa muda mrefu wa mpango huu.Na mashinani mashinani jana tarehe 7 Aprili hapa Umoja wa Mataifa kumefanyika kumbukizi ya miaka 31 ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda ambapo mmoja wa wazungumzaji alikuwa Germaine Tuyisenge Müller, manusura wa mauaji hayo na wakati huo alikuwa na umri wa miaka 9 wakiishi mji mkuu Kigali.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Duration:00:11:50