Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu-logo

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

United Nations

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Location:

New Rochelle, NY

Description:

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Twitter:

@HabarizaUN

Language:

Swahili

Contact:

9178215291


Episodes
Ask host to enable sharing for playback control

AI na teknolojia za kidijitali zaweza kuwa chachu ya kuhakikisha afya na usalama kazini - ILO

4/28/2025
Leo ni Siku ya Kimataifa ya Usalama na Afya Kazini mwaka huu ikibeba maudhui “Mapinduzi ya usalama na afya Kazini: Nafasi ya Akili mnemba na teknnolojia ya kidijitali mahala pa kazi” lengo likiwa kudhihirisha nguvu ya AI na teknolojia zinapotumika vyema zinaweza kuleta mabadiliko kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kazi duniani ILO. Flora Nducha na taarifa zaidi.

Duration:00:02:58

Ask host to enable sharing for playback control

28 APRILI 2025

4/28/2025
Hii leo jaridani tunaangazia siku ya Kimataifa ya Usalama na Afya Kazini, na juhudi za Umoja wa Mataifa za kusaidia wakulima Sudan Kusini kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Makala tunasalia na usalama kazini na mashinani tunakwenda nchini Kenya, kulikoni?Leo ni Siku ya Kimataifa ya Usalama na Afya Kazini mwaka huu ikibeba maudhui “Mapinduzi ya usalama na afya Kazini: Nafasi ya Akili mnemba na teknnolojia ya kidijitali mahala pa kazi” lengo likiwa kudhihirisha nguvu ya AI na teknolojia zinapotumika vyema zinaweza kuleta mabadiliko kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kazi duniani ILO.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP nchini Sudan Kusini chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Korea KOICA wanaendesha mradi wa kusaidia wananchi katika kilimo ili kujenga ustahimilivu na kupambana na utapiamlo. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Evarist Mapesa.Makala tunabisha hodi nchini Indonesia, taifa hili la Kusini-Mashariki mwa bara la Asia, kubwa hasa ni kumulika ni kwa vipi sekta ya uvuvi nchini humu inatekeleza kivitendo wito wa shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi, ILO kuhusu usalama na afya Kazini. Na katika mashinani fursa ni yake Abdikani Haji Hassan kutoka kambi ya wakimbizi ya Daadab iliyoko katika kaunti ya Garissa nchini Kenya ambaye kupitia Mpango wa Prospects unaoungwa mkono na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF amejikwamua kimaisha na sasa ana ndoto ya kuenda ng'ambo ili kuendeleza ujuzi wake wa kupiga picha.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Duration:00:10:39

Ask host to enable sharing for playback control

Kampuni Indonesia zachukua hatua kuimarisha usalama na afya pahala pa kazi

4/28/2025
Huko mashariki mwa Indonesia, kampuni za usindikaji samaki za PT Chen Woo Fisheries na PT Harta Samudra zimeongeza motisha wa kazi miongoni mwa wafanyakazi wake baada ya kuchukua hatua za kuimarisha usalama na afya pahala pa kazi. Hatua hizo ambazo zimeweka mazingira ya staha pahala pa kazi zinafuatia mradi wa pamoja wa shirika la Umoja wa Mataifa la kazi, ILO na Umoja wa Kampuni za Uvuvi na Usindikaji Samaki nchini Indonesia, AP2H1. ILOKampuni Indonesia zachukua hatua kuimarisha usalama na afya pahala pa kazi kupitia mafunzo.Je nini kilifanyika na hali sasa iko vipi? Assumpta Massoi anafafanua zaidi katika makala hii inayoletwa leo hii ikiwa ni siku ya kimataifa ya usalama na afya pahala pa kazi.

Duration:00:03:32

Ask host to enable sharing for playback control

WFP yasaidia wananchi Sudan Kusini kupambana na mabadiliko ya tabianchi

4/28/2025
Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP nchini Sudan Kusini chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Korea KOICA wanaendesha mradi wa kusaidia wananchi katika kilimo ili kujenga ustahimilivu na kupambana na utapiamlo. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Evarist Mapesa.

Duration:00:01:46

Ask host to enable sharing for playback control

Chanjo imepunguza vifo na maambukizi ya malaria Kenya

4/25/2025
Ikiwa leo ni siku ya malaria duniani mwaka huu ikibeba maudhui ““Malaria inatokomezwa na sisi: wekeza upya, fikiria upya, chochea upya” shirika la afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO limetoa wito wa kuongeza juhudi mara dufu na kutumia kila mbinu kutokomeza ugonjwa huo hatari unaoathiri mamilioni ya watu kila mwaka na kusababisha maelfu kwa maefu ya vifo. Moja ya mbinu hizo ni chanjo ambayo nchini Kenya imeanza kuzaa matunda kama anavyofafanua mwandishi wetu wa Nairobi Thelma Mwadzaya katika makala hii.

Duration:00:03:27

Ask host to enable sharing for playback control

Uelewa wa Hakibunifu bado ni mdogo lakini ni jambo muhimu sana ulimwenguni – Wakili Joshua Msambila

4/25/2025
Kesho Aprili 26 ni Siku ya Kimataifa ya Hakibunifu - Siku ambayo ni fursa kwa ulimwengu kukumbushwa umuhimu wa haki kwa watu wanaobuni mambo mbalimbali duniani. Ili kufahamu zaidi kuhusu Hakibunifu tumezungumza na mtaalamu wa Sheria za Sanaa na Hakimiliki, Wakili Joshua Msambila wa nchini Tanzania, kwanza anaeleza kilichomsukuma yeye kujikita katika eneo hili la sheria.

Duration:00:02:26

Ask host to enable sharing for playback control

25 APRILI 2025

4/25/2025
Hii leo jaridani tunaangazia wakimbizi wa DRC waliokimbilia Burundi, na ujumbe wa Siku ya Kimataifa ya Hakibunifu. Makala inatupeleka nchini Kenya kuangazia ugonjwa wa malaria na mashinani tunasalia hapa makao makuu katika mkutano wa Jukwaa la watu wa asili.Mazingira ya maisha kwa wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC waliongia Burundi na kupelekwa katika kambi ya wakimbizi ya Musenyi si endelevu na yanatishia mustakabali wao. Msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR Ayaki Ito, amesema hayo leo huko Geneva, Uswisi wakati akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu hali ya wakimbizi hao wanaoendelea kumiminika nchini Burundi.Kesho Aprili 26 ni Siku ya Kimataifa ya Hakibunifu - Siku ambayo ni fursa kwa ulimwengu kukumbushwa umuhimu wa haki kwa watu wanaobuni mambo mbalimbali duniani. Ili kufahamu zaidi kuhusu Hakibunifu tumezungumza na mtaalamu wa Sheria za Sanaa na Hakimiliki, Wakili Joshua Msambila wa nchini Tanzania, kwanza anaeleza kilichomsukuma yeye kujikita katika eneo hili la sheria.”Makala hii leo ikiwa ni siku ya Malaria duniani tunaelekea Kenya kwa mwandishi wetu Thelma Mwadzaya akiangazia juhudi zinazofanyika kupitia chanjo ili kupambana na malaria ugonjwa mbao Shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO linasema mwaka 2023 pekee ulikatili maisha ya watu 597,000 na na asilimia 95 ya vifo hivyo vilitokea barani Afrika, na sasa linataka juhudi mara dufu zifanyike ili kuutokomeza.Na katika mashinanin fursa ni yake Kulet Adam Ole Mwarabu kiongozi wa jamii ya kimaasai kutoka Tanzania anayeshiriki katika mkutano wa Jukwaa la watu wa asili kutoka hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa na anatoa wito wa maendelo, amani na utunzaji wa ardhi na mazingira kwa jamii ya asili na dunia nzima kwa jumla.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Duration:00:10:57

Ask host to enable sharing for playback control

‘Nenda rudi’ ya wakimbizi wa DR Congo nchini Burundi mazingira ya kuishi yakiendelea kuwa tete

4/25/2025
Mazingira ya maisha kwa wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC waliongia Burundi na kupelekwa katika kambi ya wakimbizi ya Musenyi si endelevu huku wengine wakifanya safari za nenda rudi wakivuka mto uliosheheni viboko na mamba. Taarifa zaidi na Selina Jerobon.

Duration:00:02:02

Ask host to enable sharing for playback control

Chata ya Umoja wa Mataifa inasongesha amani, maendeleo, urafiki na haki za binadamu - Balozi Yabesh Monari

4/24/2025
Tarehe 25 mwezi Aprili kila mwaka ni siku ya kimataifa ya wajumbe wanaowakilisha nchi zao kwenye Umoja wa Mataifa. Tarehe hiyo mwaka 1945 ndio ulianza mkutano huko San Francisco, Marekani wa wajumbe 850 kutoka nchi 50 waliopitisha Chata ya Umoja wa Mataifa ikilenga kusongesha amani, maendeleo, urafiki na haki za binadamu. Kama unavyofahamu Umoja wa Mataifa sasa umekua na idadi ya wanachama ni 193 na kila moja hupeleka wawakilishi kufanikisha utekelezaij wa malengo ya Umoja huo. Lengo la siku ni kuwatambua kwani wao ndio wamepewa jukumu la kufanikisha chata hiyo. Je wajumbe hao hufanya nini? Assumpta Massoi amezungumza na Balozi Yabesh Monari wa Kenya kwenye mada hii kwa kina.

Duration:00:06:42

Ask host to enable sharing for playback control

Jifunze Kiswahili: Matumizi ya maneno "MKALIMANI NA MFASIRI"

4/24/2025
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili mtaalam wetu leo ni Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua matumizi ya maneno "MKALIMANI NA MFASIRI."

Duration:00:01:12

Ask host to enable sharing for playback control

24 APRILI 2025

4/24/2025
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika Chata ya Umoja wa Mataifa inayolenga kusongesha amani, maendeleo, urafiki na haki za binadamu. Je, wajumbe wa Umoja wa Mataifa hufanya nini? Assumpta Massoi amezungumza na mmjoa wao Balozi Yabesh Monari wa Kenya, lakini kwanza ni muhtasari wa habari na ufafanuzi wa maneno.Mratibu wa misaada ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa nchini Ukraine, Matthias Schmale, amelaani vikali shambulio jipya la Urusi dhidi Ukraine lililosababisha vifo na majeruhi kwa raia, wakiwemo watoto na mwanamke mjamzito. Bwana Schmale amesema shambulio hilo la usiku wa kuamkia leo katika maeneo ya makazi jijini Kyiv na maeneo ya jirani ni ukiukaji wa kutisha wa sheria za kimataifa za kibinadamu na kwamba matumizi haya ya nguvu yasiyo na maana lazima yakome.Wiki ya Chanjo Duniani ikiwaimeanza leo, mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la afya duniani, WHO, na la kuhudumia Watoto, UNICEF, na Ubia wa chanjo duniani, Gavi wametoa onyo kwamba milipuko ya magonjwa yanayozuilika kwa chanjo inaongezeka kwa kasi. Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dkt. Tedros Ghebreyesus, anasema, “Chanjo zimeokoa maisha ya watu zaidi ya milioni 150 katika kipindi cha miongo mitano iliyopita. Kupunguzwa kwa ufadhili wa afya ya kimataifa kumeweka hatarini mafanikio haya yaliyopatikana kwa juhudi kubwa.”Na ikiwa pia leo Siku ya kimataifa wasichana katika Teknolojia ya mawasiliano, ICT, Mshauri wa masoko ya kidijitali nchini Kenya Maryann Mwangi akizungumza na washirika wetu Redio Domus amehimiza wasichana kujikita kwenye ICT kwani huu ndio mustakabali.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili mtaalam wetu leo ni Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua matumizi ya maneno "MKALIMANI NA MFASIRI"Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Duration:00:11:35

Ask host to enable sharing for playback control

Anna Ndiko: Mfuko wa ERETO tunawezesha mashirika ya watu wa asili Afrika Mashariki kutetea haki za ardhi

4/23/2025
Mkutano wa 24 wa Jukwaa la Kudumu la Watu wa jamii za asili (UNPFII) hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa linaendelea kujadili utekelezaji wa Azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watu wa asili na kubaini mbinu bora za kushughulikia changamoto zinazowakabili. Miongoni mwa shiriki wa jukwaa hilo nimwakilishii wa Shirika la Ereto Solidarity Funds ambaye amepata fursa ya kuzungumza na Sharon Jebichii wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa. Anaanza kwa kujitambulisha

Duration:00:02:28

Ask host to enable sharing for playback control

Ujumbe wa Ernest Makulilo kuhusu siku ya Kimataifa ya Kitabu na Haki Miliki

4/23/2025
Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Kitabu na Haki Miliki ambapo kila mwaka tarehe kama ya leo siku hii huadhimishwa ili kutambua nguvu ya vitabu kama daraja kati ya vizazi na vizazi na tamaduni mbalimbali. Katika makala hii Anold Kayanda wa Idhaa hii amezungumza na mwandishi maarufu wa vitabu vya elimu, Uchumi na uhamiaji, Ernest Makulilo mkazi wa Marekani katika jimbo la Missouri, kuhusu siku ya leo iliyoanzishwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO mnamo mwaka 1995.

Duration:00:03:31

Ask host to enable sharing for playback control

Nzi, panya watapakaa Gaza, UNRWA yahaha kuchukua hatua

4/23/2025
Hali si hali huko Ukanda wa Gaza eneo la Palestina linalokaliwa na Israeli ambako wakimbizi wa ndani wanakabiliwa na hatari za kiafya ambako panya na wadudu kama vile viroboto na nzi wamesambaa kutokana na mlundikano wa taka na ukosefu wa huduma muhimu kama vile maji safi na salama. Assumpta Massoi anaelezea zaidi.

Duration:00:01:42

Ask host to enable sharing for playback control

23 APRILI 2025

4/23/2025
Hii leo jaridani tunaangazia hali ya kibinadamu katika ukanda wa Gaza, na harakati za utekelezaji wa Azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watu wa asili. Makala tunasalia hapa hapa makao makuu na mashinani tunakwenda nchini Burundi, kulikoni?Hali si hali huko Ukanda wa Gaza eneo la Palestina linalokaliwa na Israeli ambako wakimbizi wa ndani wanakabiliwa na hatari za kiafya ambako panya na wadudu kama vile viroboto na nzi wamesambaa kutokana na mlundikano wa taka na ukosefu wa huduma muhimu kama vile maji safi na salama.Hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, mkutano wa 24 wa Jukwaa la Kudumu la Watu wa jamii za asili (UNPFII) linaendelea kujadili utekelezaji wa Azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watu wa asili na kubaini mbinu bora za kushughulikia changamoto zinazowakabili. Miongoni mwa shiriki wa jukwaa hilo nimwakilishii wa Shirika la Ereto Solidarity Funds ambaye amepata fursa ya kuzungumza na Sharon Jebichii wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa.Makala ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Kitabu na Haki Miliki ambapo kila mwaka tarehe kama ya leo siku hii huadhimishwa ili kutambua nguvu ya vitabu kama daraja kati ya vizazi na vizazi na tamaduni mbalimbali. Anold Kayanda wa Idhaa hii amezungumza na mwandishi maarufu wa vitabu vya elimu, Uchumi na uhamiaji, Ernest Makulilo mkazi wa Marekani katika jimbo la Missouri.Na mashinani kupitia video iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO fursa ni yake Meena Poudel kutoka nchini Nepal, Kusini mwa Asia ambaye ni Katibu wa kikundi cha wanawake watumiaji wa msitu ambacho kinabadilisha takataka za misitu kuwa mbolea rafiki kwa mazingira huku pia wakijipatia kipato."Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!

Duration:00:11:15

Ask host to enable sharing for playback control

22 APRILI 2025

4/22/2025
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo inatupeleka Msasani nchini Tanzania kusikia namna vijana na serikali wanavyolinda Mama Dunia. Pia tunakuletea muhtasari wa habari ujumbe wa Katibu Mkuu, watoto kulinda mazingira DRC, na kifo cha Papa Francis.Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya Mama Dunia, ikilenga kuchagiza hatua ya kuhifadhi sayari dunia, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametumia neno ‘homa’ kuwa inakumba dunia hivi sasa kutokana na viwango vya joto vinavyoongezeka kila mwaka. Hata hivyo amesema majawabu ya kutibu homa hiyo yapo ikiwemo kutumia nishati rejelezi ambayo ni rahisi, ina afya na salama kuliko nishati kisukuku.Huko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kando ya mapigano yanayotikisa eneo la mashariki mwa nchi, watoto wamechukua hatua kulinda sayari dunia kwa kuhifadhi misitu kwenye taifa hilo ambako ukataji miti kiholela umefurutu ada.Kufuatia kifo cha Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis hapo jana Jumatatu, ambaye maziko yake yamepangwa kufanyika Jumamosi wiki hii, mashirika ya Umoja wa Mataifa yameendelea kukumbuka mchango wake wa kutetea walio taabuni. Mathalani shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi, UNHCR limekumbuka wito wake wa kutaka kila mtu kukaribisha, kusindikiza na kujumuisha wale wote wanaobisha hodi kwenye milango yao.Na mashinani kupitia video iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO fursa ni yake Meena Poudel kutoka nchini Nepal, Kusini mwa Asia ambaye ni Katibu wa kikundi cha wanawake watumiaji wa msitu ambacho kinabadilisha takataka za misitu kuwa mbolea rafiki kwa mazingira huku pia wakijipatia kipato."Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Duration:00:09:56

Ask host to enable sharing for playback control

Uhaba wa fedha watishia ukarimu wa Zambia kwa wakimbizi - UNHCR

4/16/2025
Zambia inaendelea kuwahifadhi zaidi ya wakimbizi 106,000, wengi wao wakiwa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Burundi, pamoja na wakimbizi wa zamani kutoka Rwanda na Angola, kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR, ambalo limesema kwa kuzingatia sera yake jumuishi, nchi hiyo inakuza mshikamano na wakimbizi na kuwawezesha kujitegemea kupitia makazi maalum na ushirikiano na jamii za wenyeji. Flora Nducha na taarifa zaidi Shirika hilo la wakimbizi limesema katika makazi kama Mayukwayukwa na Maheba ambayo ni moja ya kambi kubwa zaidi ya wakimbizi nchini Zambia familia za wakimbizi zilizolazimika kukimbia makwao zinajumuishwa ili ziweze kujikimu na kuishi kwa utangamano na wenyeji wanaowahifadhi. Moulid Hujale, ni afisa habari msaidizi wa UNHCR anasema “Selikali ya Zambia inajumuisha wakimbizi katika huduma za kitaifa kama vile elimu na hata programu za msaada wa kilimo ili kuongeza uzalishaji” Amebainisha kuwa kwa kufanya hivyo Zambia imeonesha mshikamano wa dhati kwa jamii hizo za wakimbizi kwa kuhakikisha kuwa wanapata fursa ya kujenga upya maisha yao, kujikwamua kiuchumi na kuishi kwa heshima.Hata hivyo, UNHCR inasema nchi hiyo ya Kusini mwa Afrika pamoja na ukarimu wake bado inakumbwa na athari za ukame mkali uliotishia uhakika wa chakula na kuyumbisha uchumi na katika hatua za kukabiliana na hali hiyo, Moulid ansema “UNHCR inashirikiana na serikali ya Zambia kuunganisha makazi ya wakimbizi kwenye gridi ya taifa ya umeme. Tunajua muundo huu wa ujumuishwaji na maisha endelevu vinagharimu fedha, Lakini hiki ndicho hasa wakimbizi wanachokihitaji, hivyo tunahitaji msaada wako ili kufanikisha hili”. Licha ya mafanikio yaliyopatikana hadi sasa Zambia katika kuwakirimu wakimbizi, UNHCR imeonya kuwa uhaba wa fedha inaokabiliwa nao unatishia kuathiri mafanikio hayo na hasa utoaji wa huduma muhimu kwa familia hizo zilizolazimika kufungasha virago na kusaka usalama Zambia. Sasa limetoa ombi la msaada wa haraka wa kimataifa ili kuendelea kufanikisha huduma za kuokoa maisha zinazohitajika sana na wakimbizi hao.

Duration:00:02:05

Ask host to enable sharing for playback control

16 APRILI 2025

4/16/2025
Hii leo jaridani Assumpta Massoi anamulika masuala ya afya hususan harakati za kukabiliana na majanga yajayo ya afya; wakimbizi huko Zambia ambako sera jumuishi zimewajengea uwezo; Jukwaa la vijana na mchango wa sanaa kwenye usawa na utengamano. Baada ya zaidi ya miaka mitatu ya mazungumzo ya kina, hatimaye leo huko mjini Geneva, Uswisi, nchi wanachama wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) zimekamilisha rasimu ya makubaliano ambayo itawasilishwa katika Mkutano wa Afya Duniani mwezi ujao wa Mei. Pendekezo hili linakusudia kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika kuzuia, kujiandaa na kukabiliana na vitisho vya majanga ya kiafya yajayo. Anold Kayanda amefuatilia anatujulisha zaidi.Zambia inaendelea kuwahifadhi zaidi ya wakimbizi 106,000, wengi wao wakiwa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Burundi, pamoja na wakimbizi wa zamani kutoka Rwanda na Angola. Limesema shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR, likiongeza kwamba kwa kuzingatia sera jumuishi ya Zambia, taifa hilo linakuza mshikamano na wakimbizi na kuwawezesha kujitegemea kupitia makazi maalum na ushirikiano na jamii za wenyeji. Flora Nducha na taarifa zaidi.Jukwaa la Vijana la Baraza la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Kiuchumi na Kijamii (ECOSOC) limeanza jana hapa katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa na litamalizika kesho tarehe 17 Aprili. Vijana kutoka nchi mbalimbali wamehudhuria jukwaa hilo akiwemo Kapwani Kavenuke kutoka nchini Tanzania ambaye amehojiwa na Leah Mushi wa Idhaa hii. Kapwani anaanza kwa kueleza umuhimu wa mikutano hii.Gislain Kalwira, Muandaaji wa tamasha la Musika na Kipaji nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC linalofanyika kila mwaka kuleta pamoja wasanii wa kike na wa kiume wa fani mbalimbali, kwa kutambua kuwa jana dunia imeadhimisha siku ya sanaa duniani. Kalwira kupitia video iliyochapishwa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini DRC, MONUSCO, anafafanua mantiki ya tamasha hilo na kujenga usawa kijinsia.

Duration:00:09:57

Ask host to enable sharing for playback control

Wanachama wa WHO wachukua hatua za kujenga uwezo dhidi ya majanga yajayo ya afya

4/16/2025
Baada ya zaidi ya miaka mitatu ya mazungumzo ya kina, hatimaye leo Geneva, Uswisi, Nchi Wanachama wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) zimekamilisha rasimu ya makubaliano ambayo itawasilishwa katika Mkutano wa Afya Duniani mwezi Mei mwaka huu wa 2025. Pendekezo hili linakusudia kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika kuzuia, kujiandaa na kukabiliana na vitisho vya majanga ya kiafya yajayo. Anold Kayanda amefuatilia anatujulisha zaidi. "Leo mataifa ya dunia yameandika historia mjini Geneva," amesema Dkt. Tedros Ghebreyesus, Mkurugenzi Mkuu wa WHO na kuongeza kwamba, "kwa kufikia makubaliano kuhusu Mkataba wa Majanga ya kiafya, siyo tu wameweka msingi wa makubaliano ya kizazi hiki yanayolenga kuifanya dunia kuwa salama zaidi, bali pia wameonesha kuwa ushirikiano wa kimataifa bado uko hai, na kwamba hata katika dunia iliyogawanyika, mataifa bado yanaweza kushirikiana kutafuta mwafaka na mwitikio wa pamoja dhidi ya vitisho vya pamoja.” Mwezi Desemba mwaka 2021, wakati janga la COVID-19 likiwa limepamba moto, Nchi Wanachama wa WHO ziliunda Mamlaka ya Majadiliano ya Kiserikali ili kuandaa na kujadiliana kuhusu mkataba, makubaliano au nyenzo nyingine ya kimataifa, chini ya Katiba ya WHO, kwa ajili ya kuimarisha uzuiaji, maandalizi na hatua dhidi ya majanga ya kiafya. Mapendekezo katika rasimu iliyotayarishwa ni pamoja na: kuchukua hatua madhubuti za kuzuia majanga ya kiafya kwa kutumia mbinu ya Afya Moja; kujenga uwezo wa utafiti na maendeleo katika maeneo mbalimbali duniani; kuwezesha uhamishaji wa teknolojia na maarifa, ujuzi na utaalamu unaohusiana na uzalishaji wa bidhaa za afya zinazohusiana na majanga ya kiafya; kuchukua hatua madhubuti za kuimarisha maandalizi, utayari na uimara wa mifumo ya afya; na kuanzisha mtandao wa kimataifa wa mnyororo wa usambazaji na vifaa. Pendekezo hilo linathibitisha mamlaka ya nchi kushughulikia masuala ya afya ya umma ndani ya mipaka yao bila kuingiliwa.

Duration:00:01:50

Ask host to enable sharing for playback control

Jamii inapaswa kusikiliza na kujifunza kutoka kwa vijana

4/16/2025
Jukwaa la Vijana la Baraza la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Kiuchumi na Kijamii (ECOSOC) linafanyika katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani ambapo limeanza tarehe 15 Aprili na linatarajiwa kukamilika tarehe 17 Aprili 2025. Vijana kutoka nchi mbalimbali pamoja na wadau wengine wa masuala ya maendeleo na Uchumi wanakuja pamoja kujadili changamoto mbalimbali na namna bora ya kupatia ufumbuzi katika kuubadilisha ulimwengu kuwa mahali penye usawa zaidi na endelevu chini ya mwongozo wa Ajenda ya mwaka 2030 na Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs). Miongoni mwa wanaohudhuria jukwaa hilo ni Kapwani Kavenuke kutoka nchini Tanzania ambaye amefanyiwa mahojiano na Leah Mushi na hapa anaanza kwa kueleza umuhimu wa mikutano huo.

Duration:00:03:42